ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 23, 2012

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YASHIRIKI VYEMA MAADHIMISHO YA WIKI YA USALAMA BARABARANI



Mjumbe wa kamati ya usalama barabarani ambaye pia ni afisa uhusiano manispaa ya Ilala Bi.Tabu Shaibu akipokea cheti cha utendaji kazi kutoka kwa mkuu wa wilaya Ilala Raymond Mushi mara baada ya kufunga maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam jana
Mwakishi kutoka kampuni ya bia Serengeti Bw.Raymond Samwel akipokea cheti kutoka kwa mkuu wa wilaya Ilala Raymond Mushi maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam jana (wapili kutoka kulia) ni diwani wa kata ya Upanga Sultan Salim (wa tatu kulia)kaimu mwenyekiti wa kamati usalama barabarani Bw.Jeremia Makorere(wa kwanza kushoto)Stafu ofisa kamanda maalum usalama barabarani Marry Claudi
Mkuu wa wilaya Ilala Raymond Mushi kushoto)akipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya bia Serengeti Bw. Raymond Samwel alipotembelea banda hilo wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam yaliyofungwa jana (katikati) mwakilishi wa kampuni ya bia serengeti Bi.Catherine Peter(wakwanza kulia mwakilishi wa kampuni hiyo Bi.Hellen David.
Waendesha pikipiki bodaboda wakiwasili katika viwanja vya mnazi mmoja wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyofungwa rasmi jana
Hiki ndiyo cheti cha kampuni ya bia serengeti ambacho Baraza la Usalama Barabarani limeipatia kutambua mchango wao katika mapamano ya kuelimisha na kupambana na ajali za barabarani.

Dar Es Salaam Yetu

No comments: