hawa ndio warembo watakao panda kesho kwenye kinyanganiro cha Ress miss kanda ya kaskazini
JUMLA ya Warembo 11 wameingia kambini Jijini Arusha kujifua kwaajili
ya shindano la Redd’s Miss Kanda ya Kaskazini linalotaraji kufanyika
jumamosi Septemba 8, 2012 jijini Arusha.Warembo hao watapanda jukwaani katika Hoteli ya Naura Spring mjini humo kuwania taji hilo linalo shikiliwa na mrembo Syacy Alfred ambaye alinyakua taji la Mrembo mwenye Haiba ya Picha (Miss Photogenic 2011) katika Shindano la Miss Tanzania 2011.
Mwandaaji wa shindano hilo kupitia kampuni ya Jazz Promotions, Emma Mroso amesema kuwa maandalizi yote ya shindano hilo yanakwenda vyema na warembo wapo katika afya njema.
Aidha Mroso amewataja warembo walioingia kambini na wanaendelea na mazoezi yao kuwa ni Mishi Mziray, Dalina Hashim, Anita Mboya, Highmanna Lyimo, Anande Radhiel, Waridi Frenk, Buya Ernest, Lucy Stephano, Neyla Hashim, Trovina Mpanda na Theresia Kimolo.
Mratibu huyo amesema kuwa warembo hao walistaili kuwa 12 ikiwa ni warembo 3 kila mkoa kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Moshi na Tanga ispokuwa mshiriki mmoja Sara Benjamin anaumwa na yupo Nairobi kwa matibabu.
Shindano hilo linataraji kupambwa na burudani kali kutoka kwa Banan Zoro na kundi zima la B Band pamoja na wasanii wengine mbalimbali wa jijini Arusha.
CHANZO LIBENEKE LA KASKAZINI
No comments:
Post a Comment