BAADHI ya wafanyakazi wa Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) wameomba serikali kusitisha huduma za usafirisha, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ubovu wa reli na mabehewa.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na wafanyakazi wa shirika hilo mbele ya Meneja Mkuu wa Tazara, Abdallah Shekimweri.
Walisema ifikie wakati serikali iangalia uwezekano wa kusitiha huduma ya usafiri wa treni la abiria hadi watakapofanyia matengenezo mabehewa, ili kuchukua tahadhari kabla ya ajali kutokea.
“Tulituma wajumbe Makao Makuu Dar es Salaam kuomba matengenezo ya njia za reli, mabehewa lakini hatujapata majibu ya kuridhisha hivyo tunaomba Waziri wa Uchukuzi kusikia kilio chetu,” walisema na kuongeza:
“Hali ya usafiri wa reli siyo salama na kutokana na ubovu wa baadhi ya maeneo, ifikie wakati serikali kutopuuza haya tunayoeleza, ni vyema kuchukua hatua za haraka kudhibiti kabla ya majanga kujitokeza.”

Kwa upande wake, Shekimweri alikiri kuwapo kwa changamoto hizo na kwamba, tayari wamewasilisha malalamiko ofisi husika hivyo ataendelea kukumbusha serikali.
No comments:
Post a Comment