TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NOVEMBA 22, 2012
Masahihisho ya picha iliyotolewa na gazeti la Uhuru wakati bondia Onesmo Ngowi na David Migeke wakitia sahihi mkataba baina yao wa kupigana pambano lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-Es-Salaam ni mwaka 1983 na sio 1987.
Onesmo Ngowi alimdunda David Migeke kwa KO raundi ya 2 (pili) katika mpambano ulioandaliwa na kampuni ya Safari Sound Promotions ya jijini Dar-Es-Salaam ambayo ilikuwa inamiliki bendi ya musiki ya Orchestra Safari Sound chini ya mfanyabiashara maarufu bwana Hugo Kisima wa jijiniDar-Es-Salaam.
Wafadhili wakuu wa mpambano huo walikuwa Tanzania Bottlers (Coca Cola), Tanzania Distilleries (Konyagi), Kamin Industries na Chibuku.
Baada ya mpambano huo ambao ulikuwa moja ya mapambano mengi ya ushindi kwa Onesmo Ngowi alipata nafasi ya kugombea mkanda mpya wa Afrika Mashariki na Kati jijini Nairobi Kenya akichuana na bondia wa Kenya aliyekuwa anapigana ngumi nchini Japan Modest Napunyi Odour, June 1983. Mpambano huo ndio ulioanzisha ngumi za kulipwa nchini Kenya na Uganda.
Ngowi alihamia Nairobi, Kenya Septemba 1983 na kuondoka mwaka mmoja baadaye Decemba 1984 na kuhamia barani Ulaya katika nchi ya Ugiriki ambako alicheza ngumi chini ya Kampuni ya bingwa wa mieleka Ulaya George Tromaras (Tromaras Sports Arena) na kustaafu mwaka 1988 akiwa ameshamia nchini Denmark!
Imetumwa na:
Onesmo Ngowi
No comments:
Post a Comment