Tuesday, March 26, 2013

Chadema walaani kufungwa diwani wake aliyetiwa hatiani

Geita. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  mkoani Geita kimelaani vikali kitendo cha kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela diwani wa Kata ya Kasamwa mkoani humo kupitia chama hicho, Fabian Mahenge .
Diwani huyo ambaye alihukumiwa jela kwa kosa la kushiriki kuchoma nyumba za wananchi 17 katika Kijiji cha Kasamwa.
Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Chadema mkoani humo Rogers Rutunga alisema kuwa hukumu aliyopewa diwani huyo haikustahili kutokona na kosa lenyewe kuwa dogo.
“Hukumu ya miaka mitatu kwa kosa la kuchoma nyumba ni kubwa haikupaswa apewe hukumu hiyo, hilo kosa ni dogo niseme sisi kama Chadema hatujaridhika na hukumu hiyo na tuko tayari kukata rufaa, na mimi nitasimamia rufaa hiyo,” alisema Rutunga.

No comments: