Fatma Gharib Bilar,Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo, Vijana, Wanawake na Watoto- Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitoa mada wakati wa mkutano wa pembezoni ( side- Event) ulioandaliwa na wajumbe wa Tanzania Visiwani wanaohudhuria Mkutano wa 57 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake, katika mkutano huo ujumbe huo wa Zanzibar ulielezea uzoefu wake, mafanikio na changamoto mbalimbali katika kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia Visiwani humo. Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa makundi mbalimbali ya kijamii wakiwamo viongozi wa serikali, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge, vyama vya hiari, wananchi wa kawaida waume kwa wake na zaidi Viongozi wa Madhehebu yote ya Dini ili kufanikisha vita hivyo dhidi ya unyanyasaji wa wanawake na watoto. Kushoto kwake ni Bi Fatma Omar naye kutoka Zanzibar na kulia ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi.
-Bi. Mira Ihalainen, Mratibu wa Mipango kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa, UN- WOMEN ambaye alikuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu, katika mazungumzo yake, Bi Mira alieleza pamoja na mambo mengine kwamba UN- WOMEN itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano ikiwa ni pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kiufundi na kitaalam katika shughuli zote zinazolenga kumkomboa mwanamke na mtoto wa kike. kulia kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ( Tanzania Bara), Bi. Kijakazi Mtengwa akifuatilia majadiliano hayo na kushoto kwa Mira ni Afisa Ubalozi, Modest Mero aliyekuwa mratibu wa wa majadiliano.
Fatma Gharib Bilar, Katibu Mkuu , Wizara ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, amesema, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, wanayo nafasi kubwa na ya muhimu katika kukabiliana na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike.
Ameyasema hayo jana jumatatu wakati ujumbe wa Tanzania Visiwani, unaoshiriki mkutano wa 57 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW) ulipoanda mkutano wa pembezoni ( side event) kwa lengo la kubadilishana na washiriki wengine uzoefu wao , mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo katika kushughulikia unyanyasaji wa kijinsia Tanzania Visiwani.
Mkutano huo wa pembezoni na ambao ulivutia washiriki wengi mada yake ilikuwa “Vunja ukimya, unga mkono, juhudi za sekta mtambuka katika kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia, uzoefu wa Zanzibar”.
Kwa habari zaidi na picha, bofya read more
Akiwa msemaji mkuu wa
mkutano huo, Katibu Mkuu, Fatma Bilar
ameeleza kwamba kwa uzoefu wa wao
(Zanzibar) wamebaini kwamba, ili juhudi hizo ziweze kufanikiwa, mbali ya ushiriki wa viongozi wa serikali na
wadau wengine, viongozi wa madhehebu ya dini ni kundi ambalo lina umuhimu wa kipekee.
“ harakati zetu
zinahusisha makundi mbalimbali ya kisekta,
zikiwazo wizara, idara na taasisi
mbalimbali achilia mbali viongozi wakuu wa serikali, lakini tumetambua kwamba
hakuna dini yoyote ile inayohubiri ukatili dhidi ya wanawake, na kwa sababu
hiyo tunaamini kwamba viongozi wa madhehebu yote ya dini wanapashwa kushirikishwa
na kushiriki kikamilifu katika juhudi
hii” akasisitiza Katibu Mkuu.
Na kuongoza kwamba, viongozi hao wa madhehebu ya dini bila ya
kujali kama ni waislamu au wakristo wote wamekuwa wakijitahidi kuunga mkono
harakati hizo kwa kuwaelimisha waumini
wao kuhusu madhara ya unyanyasaji wa
kijinsia.
Akabainishwa kuwa ilichukua juhudi nyingi
ukiwamo utafiti kubaini kwamba Zanzibar kulikuwa na tatizo kubwa la
unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Akasema tafiti hizo ndizo zimewafumbua macho hata
viongozi wa serikali na mamlaka
mbalimbali na hivyo kuanza
kuchukua hatua za kulikabili tatizo
hilo.
Akaainisha juhudi
mbalimbali na baadhi ya mafanikio
yakiwamo yale ya kuanzisha makazi salama ya kuwahifadhi waathirika .
Ingawa ambayo ingawa alikiri kwamba bado kuna changamoto nyingi za uhaba wa
raslimali fedha, wataalamu na kazi kubwa ya kubadili fikra na mitazamo ya watu
kuhusu suala zima la ukatili wa kijinsia.
Washiriki wa mkutano
huo wa pembezoni baada ya maelezo
ya Katibu Mkuu walipata nafasi ya
kuuliza maswali na kupata ufafanuzi zaidi. Na Maswali yote pamoja ufafanuzi huo yalijibiwa kwa Ufasaha na
Katibu Mkuu pamoja na wajumbe
aliofuatana nao.
washiriki wakifuatilia mkutano
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wa pembezoni ulioandaliwa na ujumbe wa Tanzania Visiwani.
mjumbe akiuliza swali
wajumbe walijitokeza kwa wingi kuja kujisikilizia uzoefu wa wataalamu hawa kutoka Tanzania Visiwa
isiwe taabu wengine waliamua kujikalia chini.
Katibu Mkuu akiendelea kujibu mswali kutoka kwa washiriki waliokuwa bado na hamu ya kujifunza kutokana na uzofu wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment