ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 18, 2013

CUF: Yussuf Salim Hussein ndio Mgombea Ubunge Chambani

CUF_01
CHAMA cha Wananchi CUF kimemtaja mwanachama wake, Yussuf Salim Hussein kuwa mgombea wa nafasi ya Ubungue katika jimbo la Chambani uliopangwa kufanyika Juni 16 mwaka huu. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Uenezi wa CUF, Salum Abdalla Bimani jina la mgombea huyo limepitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho katika kikao chake cha kawaida cha siku mbili kilichoanza juzi.

Kikao hicho pamoja na mambo mengine kilijadili majina ya wagombea 12 waliojitokeza kuwania kuteuliwa na chama kuwania nafasi ya Ubunge Chambani katika mkoa wa Kusini Pemba.

Nafasi ya Ubunge jimbo la Chambani iko wazi kufuatia kufariki dunia kwa aliyekuwa Mbunge wake kupitia chama cha CUF, marehemu Salim Hemed Khamis Machi 20, mwaka huu.

Kampeni za uchaguzi huo zimepangwa kuanza Mei 18

No comments: