ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 17, 2013

FAINALI MISS UTALII TANZANIA 2013, KUFANYIKA JUMAPILI MKWAKWANI TANGA

DSCN7933
Hatimaye fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,zinafanyika mkoani Tanga siku ya Jumapili Tarehe 19-5-2013katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga. Fainali hizo za tano za Taifa za mashindano ya Miss Utalii.

Tanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, zitajumuisha jumla ya warembo 30 kutoka mikoa yote ya Tanzania, na vyuo vikuu watapanda jukwaani kuwania taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/13.

Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni mkataba wenye thamani ya sh.90, 000,000/=,ambao unajumuisha skolashipu ya kusoma kozi ya Diploma katika chuo cha Dar es Salaam City Collage, safari za kushiriki mashindano ya Dunia,ziara za Tanzania Great Safari and Tour 2013, kugharamiwa usafiri wakati wa shughuli za kutekeleza majukumu yake ya ushindi,na shilingi 5,000,000/= baada ya kutumikia taji lake wakati wa kukabidhi kwa mshindi wa msimu ujao. 

Aidha mshindi wa pili hadi wa tano, kila mmoja kila mmoja atajipatia mkataba wenye thamani ya shilingi 58,000,000/=, ambao pia unajumuisha skolaship za kusoma chuo cha Dar Es Salaam City Collage na safari za kushiriki mashindano ya kimataifa nay a dunia, pia ushiriki wa safari za Tanzania Greet Safari and Tour 2013 na kugharamiwa usafiri wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya ushindi.

Washiriki walio bakia watajipatia tuzo mbalimbali za heshima, za utalii, utamaduni, jamii, uchumi, mitindo, ,wanyama pori,misitu,mazingira,utalii wa ndani,utalii wa kitamaduni,jinsia,utalii wa michezo,utalii wa mikutano,elimu ya jamii,afya ya jamii, urembo na maliasili.

Mashindano ya Dunia ambayo washindi hao watashiriki ni Miss Tourism World 2013, Miss Tourism United Nation 2013, Miss Tourism University World 2013, Miss Heritage World 2013, Miss United Nation 2013,Miss Freedom Of The World 2013,na Miss Globe International 2013.

Burudani katika fainali za mwaka huu ,zitakazo fanyika kitaifa mkoani tanga jumapili tarehe 19-5-2013, ni pamoja na Bendi ya Msondo Ngoma, Mwana mziki wa kimataifa Che Mundu Gwao, Ngoma za asili na vichekesho kutoka kundi la Majuto Arts Group linalo ongozwa na mwigizaji mahili na mkongwe Mzee Majuto,sarakasi na muziki wa kizazi kipya yani bongo fleva.Maandalizi yamekamilika, na hali ya kambi ni shwari huku washiriki wote wakiwa katika hali ya kujiamini, kila mmoja akijigamba kupeleka jaji mkoani kwake mwaka huu.

No comments: