Wednesday, June 12, 2013

PITA PITA NEW YORK CITY WATU WAWILI WA KWAMA KWA MASAA 2 KWENYE JENGO LENYE UREFU WA FUTI 500 HEWANI.

Hearst Tower  New York City jengo lenye urefu wa Futi 500 kwenda juu sawa na ghorofa 46 lili leta kizaza  mchana wa leo baada ya wafanyakazi wakuosha madirisha kukwama pale chombo chao kilivyo vunyika kikiwa uko hewani. Wafanya kazi wa zimamoto na polisi wa New York City walifanya kazi ya ziada kuokoa maisha ya watu hao wawili waliokuwa wamekwama kwa masaa 2 hadi walivyo kuja kuokolewa wakiwa salama.
Picha hii na ya chini unaweza kuona chombo hicho kikiwa kimevunjika katikati na kusababisha maisha ya watu hao kuwa nusu kwa nusu nikiwa na maana nusu kuishi nusu kupoteza maisha.
Helicopter ya NYPD hikipita usawa wa jengo hilo lililopo 57 St na 8 ave New York   tayari kwa kuwaokoa watu hao wa wili waliokuwa wamekwama wakiwa katika harakati za kujitafutia mkate wa kila siku.
 Picha ikionyesha polisi wakiweka kamba hili watu wasikatishe sehemu hiyo hili kutoa nafasi kwa watu wa NYFD (zimamoto) waweze kufanya kazi yao.


1 comment:

Anonymous said...

kwanini wasikwamwe na wanawajiri watanzania wasiojua kujenga na waspenish si wanapenda vya bure njoo new york utaona mafundi mchwara wa kibongo hawakwenda shule basi wanafunga elevator kisa wajanja mjini