Wednesday, July 17, 2013

NAPE AKWEPA KUZUNGUMZIA MATOKEO UDIWANI ARUSHA..."WAULIZENI VIONGOZI WA CCM ARUSHA"

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema wanaopaswa kuulizwa jambo lolote linalohusu uchaguzi wa udiwani wa kata nne uliofanyika Jumapili wiki iliyopita, jijini Arusha, ni viongozi wa chama wa mkoa huo.
Nape alisema hayo alipozungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, baada ya kutakiwa kutoa maoni yake kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuibuka mshindi katika kata zote nne.
“Waulize wenyewe. Siwezi kuzungumzia issue (suala) ndogo. Unajua chama chetu kimegawa majukumu. Kule kuna mwenyekiti wa mkoa, katibu pamoja na wengineo,”alisema Nape.

Alipoulizwa sababu za kutoa maoni katika chaguzi nyingine mara tu matokeo yanapotangazwa, kama vile Jimbo la Igunga, Nape alisema uchaguzi huo unahusu ubunge tofauti na udiwani.

Alisema hata katika uchaguzi wa kata nyingine 22, alizungumza kwa kuwa ulikuwa umehusisha kata mbalimbali nchini na siyo mkoa mmoja.

1 comment:

Anonymous said...

Kwa mtazamo wangu tu mie naona Chama tawala inabidi mkaze buti, mje na sera za nguvu na mabadiliko ya haraka haraka ama sivyo mtakuwa matatani sana. Wanachotaka wananchi ni: Nchi kuwa na ulinzi wa kutosha na wa uhakika, Amani kurejea nchini haraka sana haswa mji wa Arusha, Umeme umekuwa kilio katika majimbo mengi, Maji masafi kitu ambacho ni muhimu sana mpaka leo hakuna, matibabu haya ridhishi kwasababu waganga hawalipwi mishahara mizuri, Elimu walimu hawalipwi mishahara ya kutosha hizo ni kerooo nizisikiazo kila kukicha, na uwazi katika mambo mengi bila kuficha ficha, na kuwakaba koo wezi wafedha za uma katika sekta zooooooote. Sisemi kuwa chadema watatimiza hayo yooote leo au kesho ila wanaonyesha upambanaji, wanaonyesha nyuso za matumaini. (eeeh Mwenyezi Mungu ibariki TANZANIA).