Omari Kimweri
BONDIA MTANZANIA Omari Kimweri 'Lion Boy' anaefanya shughuli zake Deer Park, Victoria, nchini Australia anatarajia kuwa mtanzania wa kwanza kupanda uringoni November 30 kugombea ubingwa wa Dunia unaotambuliwa na WBC uzito wa kg47.5 minimum weight
Mpambano huo utakaopigwa nchi ya China November 30 na bingwa wa dunia wa uzito huo nchini china
xiong zhao zhong ni bingwa wa dunia WBC minimum weight ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo
Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia uku sapoti kubwa akitegemea kutoka Tanzani ambapo alipo zaliwa
na kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kula imemdondokea bondia Omari Kimweri kwa mara ya kwanza mtanzania huyo ataonekana Dunia nzima akijaribu kuwania ubingwa wa WBC
Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi ya mwisho ya kujiandaa na mpambano huo amesema kuwa yeye bindafsi yupo tayali kabisa kwa mpambano huo kwani yeyey pia ni bingwa na katika kuzihirisha hilo ameomba watanzania waendelee kumuombea kwani uwakika wa yeyey kunyakuwa ubingwa huo ni mkubwa sana aliongeza kwa kusema ubingwa huo baada ya kuunyakuwa atakuja nchini Tanzania ili kuwaonesha mkanda huo wa ubingwa wa Dunia mana ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote
huku akitegemea zaidi duwa za watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote Mungu Ibariki Tanzania Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri
No comments:
Post a Comment