ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 4, 2013

KAMA KAWAIDA WAKENYA NA MBIO NDEFU NI SAWA NA MASAI NA BOMA LA NG'OMBE


Kenya ni moja ya nchi inayosifika kwa kutoa wakimbiaji wazuri wa mbio ndefu ambapo kila Marathon inayofanyika kokote duniani unaweza kusikia kati ya washindi kumi wa kwanza lazima kuna raia kutoka Kenya. Historia hiyo imeendelea kuandikwa tena na wakimbiaji wawili Geoffrey Mutai mwenye miaka 32 kwa upande wa wanaume na Priscah Jeptoo mwenye miaka 29 kwa upande wa wanawake kwenye New York Marathon
Kama mwaka 2002 na 2003 wanariadha kutoka Kenya walishinda mataji yote mawili kwa upande wa wanawake na wanaume, mwaka huu pia historia imejirudia kwa Priscah Jeptoo kushinda kwa wanawake kwa saa 2 dakika 25 na sekunde 07. Geoffrey Mutai pia alishinda kwa upande wa wanaume kwa kutumia saa 2 dakika 8 na sekunde 24.Kila mmoja ameshinda $500,000 kwenye mbio hizi.

Kutokana na historia ya Boston Marathon kupata uvamizi na waliotajwa kuwa ni magaidi, waandaaji wa New York Marathon wametumia zaidi ya $ 1.000.000 kwa ajili ya ulinzi. Ukaguzi maradufu kwa watazamaji ulifanyika,askari wengi waliwekwa kwenye njia zote ambazo wanariadha walikuwa wanapita. Heshima zilitolewa kwa watu wote waliathirika na shambulizi la Boston Marathon kwa wanariadha kuvaa ribbon ya blue mkononi

No comments: