Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya kwa meli ya MV Songea.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipuliza vuvuzela pamoja na wananchi wa Mbamba B
ay waliokuja kuusindikiza msafara wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana,ambao umemaliza ziara ya mkoa wa Ruvuma na kuanza safari ya kuelekea mkoa wa Mbeya .
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha -Migiro akitoa salaam za shukran kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa ukarimu wao wa muda wote wa ziara na kuwatakia maisha mema.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kabla ya kupanda meli kuelekea wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa wilaya ya Nyasa na kuwaambia serikali imeshaagiza meli ya tani 400 ambayo ipo kwenye matengenezo sasa na ikikamilika italetwa ziwani hapo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na ujumbe wake pamoja na viongozi wa CCM mkoa wa Ruvuma kabla ya kupanda meli kuelekea Kyela mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiaga wananchi wa wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma tayari kwa safari ya kuelekea Kyela mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwaaga wananchi wa wilaya ya Nyasa wakati wakiondoka kwenye bandari ya Mbamba bay kuelekea Nyasa.
"Kwa Herini wana Nyasa"msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ukiwaaga wananchi wa wilaya ya Nyasa.
Ni siku ya Kihistoria kwa CCM na Wana Nyasa kwani matumaini yameongezeka kwa wananchi hao baada ya viongozi wao wa Kitaifa kuwa nao kwa muda wa siku tisa mkoani Ruvuma.
No comments:
Post a Comment