Ndugu Washarika,
Nawasalimu Katika Jina La Yesu Mwokozi.
Kama tunavyofahamu Jumapili ndiyo siku yetu ya mavuno. Mtumishi wa Mungu Mama Chilwa Kiliaki ndiye atahubiri katika ibada. Tafadhali tujitokeze kumsikiliza mtumishi pia na kufanikisha siku hii muhimu ya mavuno. Mgeni wetu rasmi ni balozi wa Tanzania Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula. Kwa hiyo pia ni vizuri kufika kumpokea mgeni na kiongozi wetu.
Ibada itaanza saa nane kamili. Utaratibu wa kufanya shughuli ya mavuno utaanza saa tisa kamili. UNAWEZA KULETA FEDHA AU KITU CHOCHOTE AMBACHO UMEPANGA KUMTOLEA MUNGU WAKO.TUNASISITIZA WASHARIKA KULETA VITU MBALIMBALI KWA AJILI YA MNADA.
Anuani ni
2730 E 31st street
Minneapolis MN 55406.
Kutakuwa na chakula baada ya shughuli ya mavuno. Akina mama tunatanguliza shukrani kwa wale ambao tayari wamejiandikisha kuleta vyakula.Bado kuna nafasi kama hujajiandikisha unaweza kuleta chochote ambacho unajisikia kushirkiana na wenzako. Akina baba tunawaomba kuleta soda,juisi au maji.
Wazee wote wa usharika watakuwa zamu Jumapili kwa utaratibu tuliopangiana.Kwa hiyo watakuwepo kuwaelekeza na kusaidia kila itakapohitajika.
Karibuni Sana tumtolee Mungu kwa jinsi tunavyobarikiwa kila siku.Pia kumpokea balozi wetu na kiongozi wetu ambaye ametupa heshima kubwa kukubali kuwa mgeni rasmi.
Mbarikiwe Sana,
Dear Congregants.
Greetings in the Name of Our Lord Jesus Christ.
As you already know this Sunday is special harvest for our congregation.We are blessed having Gods servant Ms Chilwa Kiliaki who will deliver the Sermon.Please join us to make the day successful as it should be.Also Tanzania Ambassador in US is our guest of honour so we need to show up to give her warm reception.
The regular service begins at 2pm.AT 3pm we will then begin the harvest business. Congregants and friends can bring money or anything they feel blessed to give to God. WE REQUEST CONGREGANTS TO BRING DIFFERENT STUFF WHICH CAN BE SOLD DURING THE AUCTION AS THEIR OFFERING.
Address is
2730 E 31st street
Minneapolis MN 55406.
.
Food will be served after the official service and harvest.We thank those who have volunteered to bring food. If however you did not register and you want to bring something to share you are welcome. All men are requested to brind soft drinks like sodas,juices and water.
All ushers will be on duty Sunday to help and facilitate both the service and harvest ceremonies.
Please come bring family and friends. Spread the news to other people and let us make the harvest ceremony as it should be. Also we need to come to receive our Ambassador who has shown as she cares for accepting our invitation.
We look forward to see you,Sunday.
God Bless
Rev. Andrea Mwalilino.
No comments:
Post a Comment