ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 1, 2013

USIPOKUJA KWENYE MSIBA WAMWANAGU SIJI MSIBA WA BABAYAKO , BONGO MOVE HAO NDIO WAMESEMA.

Wema Sepetu (katikati) baada ya kuwasili Zanzibar. Kushoto ni rafiki yake Kajala Masanja.
Habari kutoka chanzo chetu makini zilidai kuwa hoja dhaifu iliyotumiwa na wahusika hao ni kwamba Wema huwa haendi kwenye misiba ya wenzake hivyo naye amzike baba yake mwenyewe.

MFANO; MSIBA WA SAJUKI
Ulitolewa mfano wa msiba wa aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2, mwaka huu ambapo Wema alidaiwa alishindwa kufika kwa sababu alikuwa studio akirekodi wimbo wake mpya ambao haujatoka hadi leo.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria mazishi ya baba'ke Wema Visiwani Zanziabar.
Wapo waliokwenda mbele zaidi na kudai kuwa hata ukifunua madaftari yao wanapopatwa na misiba huwezi kukuta jina la Wema akiwa amesaini wala kufika.
SHARO, KANUMBA
“Kwa njia moja au nyingine, Wema bwana huwa hashiriki sana katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti pale Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo Milionea (Hussein Mkieti) na (Steven) Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake.
Wema (wa sita kutoka kulia) na ndugu zake wakiwa kanisani wakati wa ibada ya kumuaga baba yao.
“Wanadai mara nyingi amekuwa akijitenga na misiba ya wenzake na wala huwa hatoi hata pole kwa wafiwa kama wafanyavyo wengine wanaposhindwa kufika msibani kutokana na sababu mbalimbali hasa za kimajukumu au kuwa safarini,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kuna habari za chinichini kuwa walikaa kikao na kukubaliana kutohudhuria msiba wa Wema. Ilitengenezwa meseji ikatumwa kwa memba wote.”
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa kiongozi wa kundi hilo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa uhamasishaji watu wasiende msibani kwa kigezo cha Wema kutojumuika na watu wengine katika matatizo yao.
 akiweka udongo katika kaburi la baba yake.
WEMA ANASEMAJE?
Akizungumzia ishu hiyo ya kususiwa msiba wa baba yake Wema alisema: “Nimesikitishwa na kitendo hicho. Nahisi siyo sahihi kwa kuwa nimekuwa nikihudhuria misiba ya watu mbalimbali.
“Hawakuwa sahihi kunifanyia hivyo katika kipindi hiki kigumu, hata hivyo, wangekuja kwanza tumzike baba ndiyo nijifunze ila kutokuja kwao hakujanipunguzia chochote.”
Kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni kama kumuongezea machozi mara mbili kwani tayari alikuwa na chozi la kuondokewa na baba yake kipenzi na la pili likawa ni kususiwa msiba.

Wema akiweka shada la maua katika kaburi la baba yake kwa simanzi.
Baada ya habari hizo kujaa tele kwenye meza ya gazeti hili, wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya mastaa wanaounda Bongo Muvi juu ya kumsusia msiba Wema ambapo kila mmoja alikuwa na utetezi wake;
Ray: Mh! Kweli Wema haendagi kwenye misiba ya watu hata mimi sikumuona kwa Sajuki ingawa sijui kama alionekana baadaye ila kwa sasa niko sehemu mbaya nitakupigia baadaye tuongee kwa kirefu.
Halima Yahya ‘Davina’: Sikwenda msibani kwa sababu na-shoot na nina mambo yangu ya kifamilia ila niliambiwa nisiende.
Steve Nyerere: Mi nilifiwa na mwanangu sikumuona Wema, tunaangalia kwenye kumbukumbu za wasanii wanaofariki dunia Wema hajawahi kuonekana. Mi’ naomba wasanii wapendane kikweli siyo kinafiki.
William Mtitu: Niko shooting wiki nzima ila kama Wema hakuonekana kwenye misiba ya watu hasa kwa Sajuki alikuwa anakosea sana. Pia alikosea kwa kuwakandia wasanii kwenye vyombo vya habari, kama walikosea angekaa nao akawaambia.
Kulwa Kikumba ‘Dude’: Nilikwenda msibani kutoa pole kwa sababu wale ni ndugu zangu lakini nilivyofiwa na mama yangu Wema hakuonekana wala hakunipa pole na huwa haonekani kwenye misiba ya wengine kama ilivyotokea kwa Sajuki ingawa mimi siwezi kulipa kisasi.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ (katikati) akishiriki mazishi ya baba mzazi wa Wema, Balozi Sepetu Visiwani Zanzibar.

ZANZIBAR; DIAMOND NDANI
Kutoka visiwani Zanzibar alikozikwa baba Wema Jumatano iliyopita, ripota wetu alimshuhudia mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiungana na wasanii wengine waliokuwa bega kwa bega kumfariji mrembo huyo.
Habari za kina zilidai kwamba kwa kuwa Diamond hakufika kwenye msiba nyumbani kwa akina Wema, Sinza-Mori, Dar ilibidi aungane na mrembo huyo visiwani Zanzibar kwani naye amekuwa akimendewa na kashfa hiyo ya kuhudhuria misiba mikubwa na kupotezea ya watu wa kawaida.
Aidha, wasanii wengine walioamua kwenda msibani bila kujali onyo la kutokwenda ni pamoja na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Elizerbeth Michael ‘Lulu’, Kajala Masanja, Mahsein Awadhi ‘Dokta Cheni’, Salumu Mchoma ‘Chiki’ na Jaqueline Wolper.
Balozi Sepetu alifariki dunia Jumapili iliyopita baada ya kusumbuliwa na kisukari na kupooza ambapo juzi Jumatano alilazwa kwenye nyumba ya milele huko visiwani Zanzibar.

KUTOKA IJUMAA
Gazeti hili linawashauri wasanii kushirikiana katika shida na raha, kusameheana wanapokoseana na kutowekeana vinyongo kwani vinaweza kusababisa mpasuko miongoni mwao.

Imeandikwa na Hamida Hassan, Gladness Mallya na Imelda Mtema

6 comments:

Anonymous said...

Hivi kweli mtu mzima na akili zako mtu mwingine anakukataza kwenda msibani na hauendi? am speechless!

Anonymous said...

yaanu kweli nimeamini baadhi ya watu wa hiyo bongo movie ni wajinga eti mnaambiwa msiende msibani nanyi mnaacha, kuanzia leo jioneni nyie wajinga, watu husameheana kwa swala la msiba. mmenishangaza sana tena bora mngenyamaza kuliko kujiongelesha ujingaaa.na mnajiita kioo cha jamii, pumbaaavu.

Anonymous said...

hao wasanii wanajichosha na ujinga ameenda kikwete na viongozi wa juu nyie vidampa ndio kina nani? watu wamejaa tele kwanza mmempunguzia mashuzi ya kuwafata kwenye mashida yenu yasiyokwisha ujinga mtupu unakwenda msiba unaokuhusu hapa mjini ukiendekeza kuzika kila anayefariki basi kazi zote zitalala sijui utakula nini

Anonymous said...

waswahili hawaishi vituko huyo kiongozi wa mgomo atakua mswazi halafu Wema kamzidi kiuwezo analeta chuki binafsi mchunguzeni muone, nawaonaga huku uswazi kwetu tunakoishi wengi hawafanyi kazi za kuajiriwa basi ukitokea msiba wewe mfanyakazi utajitahidi kutoa mchango utaenda makaburini kuzika utalala nao usiku matangani utasaidia kila kazi za hapo msibani kosa linakuja asubuhi ukienda kazini watatoa maneno ya kashfa mpaka utaogopa utasikia kaona kazi yake ya maana kuliko msiba khaa wataongea hapo mpaka mishipa ya shingo iwasimame kaenda kazini kaenda kazini kaacha msiba hivi nikiacha kazi mtanilisha nyinyi? na huo msiba aliekufa ni baba yangu mzazi mpaka niache kwenda kazini yaani hawaelewagi akili mgando kwisha kazi wanakera usiseme zamani nilikua nawamind naomba ruhusa kazini bado wanalalamika siku hizi nimejifunza naenda kazini kama kawaida nikirudi jioni naenda kuwapa pole natoa mchango yule nasepa zangu kwenda kulala nyumbani waongee vizuri tena kama msiba wanazika katikati ya wiki ndio kabisa hawanioni hata kuzika naenda kazini kama kawa nawapa pole nikirudi hawana wema kila unachofanya ni makosa basi bora yawe makosa yooote nimeacha kabisa nimebadilika nashika yangu nikifiwa ninao ndugu zangu na familia yangu hata tukiwa watu wanne tutazika tu sihitaji kujaza watu kwanza sina pesa za kuwalisha maharage ya bure pumbaff zenu

Anonymous said...

Iwe fundisho kwa wengine, yeye ni nani asiyehudhuria misiba ya wenzake. Msiba ni sehemu ya kufarijiana kama wewe huendi kufariji wenzako nao hawatakuja

Anonymous said...

It doesnt make sense either you attende the funeral or not....as the mirrow of the community you shouldnt suppose to pay back...if she hasnt attended others funeral that is her own problem...as a human being you need to be flexible... you cant satisfy everyone in this world.