Neno hili majanga nimelipata kutoka kwenye nyimbo ya sanura ambayo nimeipenda tamthilia ya methali zake. Nikinukuu moja inasema; “Kufiwa nifiwe mimi, kulia ni lie mimi, pole upokee wewe.” Akimaliza huwa anafungia semi zake kwa neno majanga.
Majanga ninayokusudia kuzungumzia leo ni majanga ya uhai wa Jumuiya za Watanzania. Watanzania tumekuwa na historia ngumu ya udumishaji Jumuiya zetu. Ugumu ambao umechangia sio tu kusitisha maendeleo ya kijamii yanayotegemea usimamizi wa mpangilio maalum. Uanzishaji wa Jumuiya ambazo mara nyingi baada ya miaka 3 hadi 5 huwa zinafifia na hata kufa, mfumo wa aina hii umechangia sana uumiza wa jamii za Watanzania, na pia zinakatisha tamaa kwa jamii zenye malengo ya kuunda Jumuiya zinazofanana na hizo zilizo kufa. Na kitu cha kushangaza sana, Watanzania tumefeli kabisa katika kujifunza juu ya kosa hili. Jamii mpya zimekuwa zikiendelea kuanzisha Jumuiya, na kurudia makosa yale yale yaliyo fanywa na jamii jirani.
Mimi nimeona haja ya kujadili suala hili na kuangalia miongoni mwa sababu ambazo labda tunaweza kuona haja ya kukuz mazingatio, ambayo labda tunawea kuleta mabadiliko katika hili.
Moja ya sababu ambazo naamini ni chanzo cha kufa Jumuiya za Watanzania ni Malengo. Mara nyingi waasisi wa Jumuiya wanapounda chombo kunatokea na miongoni mwao na ajenda za mifukoni, au ajenda za siri. Wanakuwa na Malengo yao binafsi, ya kukidhi mahitaji au matashi yao wenyewe bila kuzingatia jamii kwa ujumla. Jambo hili limeweza kuwa chanzo kikubwa cha kuleta mifarakano katika sehemu mbali mbali. Ajenda hizi huwa zinabaki vifuani mwa wenye nazo, ambazo haziwezi kuwekwa mezani ni kwa sababu haziwiani na mahitaji ya wengi.
Kadhia inaanza, wakati wa kufanya maamuzi. Hoja zinakuwa zipo wazi, wakati mwingine zinakuwa hazina utata, lakini zinaishia kutokubalika na kupingwa kwa nguvu zote na wachache au mmoja ambaye mwenye nguvu ya juu, tu kwa sababu hoja hizo zinanyima fursa ya ajenda binafsi, ambayo/zo hawezi kuzi/iweka mezani. Jitihada za kufichiana na kunyimana taarifa za zinaanza, au za kupeana taarifa zisizo na ukweli mtupu. Mmoja huyu au wachache hawa, watajenga maelezo mengi ya upingaji wa hoja. Mfarakano unaanza, mipasuko ya uongozi na hata vyombo hivi vya kijamii huishia kufa.
SULUHU; Miongoni mwa suluhishio ya hili ni kujaribu kuunda uongozi ambao haumpi madaraka mengi au makubwa sana kiongozi mmoja, na badala yake yanakuwa ni ya viongozi walio wengi. Kuhakikisha chombo cha kukuza mawasiliano na jamii, kinapewa kipaumbele sana, ili wana jamii wawe sehemu ya mchakato mzima wa maamuzi. Na pia kuhakikisha wanajumuiya wanafahamu kuwa wao ndio wenye maamuzi ya mwisho.
Katika maoni yangu yajayo; nitazungumzia jinsi gani uliliaji wa madaraka unavyochangia kuuwa Jumuiya za Watanzania,..
2 comments:
Loh! Ndugu! Nimekupenda sana kwa suala hili!
WATANZANIA tuna roho mbaya! Wakatili na tusiokuwa na haya ! You said it well! Shame on us!
Nimeshuhudia mwenyewe ugomvi Kama wa kilevi, kutoelewana bila sababu. Kukataa kukaa mezani pamoja kisa wachache wenye hila , kutaka kujitangaza na kuibia Jumuiya makusudi ! Sasa Jumuiya yetu ipo Kwenye life support, kupona, tunategemea miujiza!
Hongera ndugu!
Ushauri: Kila Jumuiya zinajengwa na kuimarika kutokana na misingi na utamaduni unaolindwa na wana Jumuiya. Nyingine zinajifunza kutokana na mapito ya matatizo na mafanikio wanajumuiya wanayoyapitia. Viongozi huchaguliwa na Jumuiya kwa kuzingatia kanuni zilizopo au zilizowekwa na wanajumuiya. Mimi ni mmoja wa wanajumuiya na nashiriki kwenye Jumuiya. Nimejifunza kuangalia mafanikio pasipo na mafanikio. Matatizo hayatakosekana kwani ni Jumuiya, yatakuwepo tuu. Naamini kuna ujumbe muhimu sana wa kuzingatia kwenye maelezo uliyoyatoa na hongera kutumia muda uliotoa kuyashirikisha kwa blog.
Changamoto:
- Ni sisi ndio wa kuyafanyia kazi mambo ya Jumuiya, kuwa na umoja na kuimarisha umoja.
- Kutambua kuna gharama za kuwa na Umoja/Jumuiya; ni sisi ndio tunahusika kuzilipia gharama hizo sasa na sio baadae.
- Kuwa tayari kujitoa kwa vizazi vya mbele ili kuwapa nafasi ya kujifunza yale mazuri yatokanayo na umoja katika Jumuiya
- Ni vizuri kuyazungumzia na ni busara kuyafanyia kazi
Post a Comment