ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 13, 2014

BARUA YA WAZI KWA MHE. PROFESA ANNA TIBAIJUKA: NHC INAHITAJI MABADILIKO YA HARAKA

Kwako Mhe. Waziri Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka (Mb)

Salaam

Mama nakuandikia wewe kama Waziri mwenye dhamana yakuongoza, ku-monitor and evaluate shirika la NHC. Natumia muda wangu kukuandikia kwakuwa najua wewe unajali, wewe ni msikivu, upo karibu sana na wananchi, ni member wa jamii forums na kikubwa kwakua najua wewe ni kiongozi progressive unaependa mabadiliko na maendeleo ndio maana umedumu katika uongozi huko UN na hata hapa nyumbani katika Jamuhuri yetu. Pia najua utasoma barua hii, itagusa, utaijibu na utaifanyia kazi kwakuwa hivyo ndivyo ulivyo na ndivyo tunavyo kufahamu sisi wananchi.

Ni ukweli usiopingika kuwa Watanzania wengi hawapendezwi na mwenendo, sera na uendeshajiwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC. Kama inavyoainishwa kwenye maoni na malalamiko machache hapa chini - yaliyotolewa na baadhi ya wakereketwa – mambo yafuatayo ndio hasa ambayo yamekuwa yakilalamikiwa sana na ambayo tunakuomba uyatafakari na kuyafanyia kazi:


Mosi: Watu wachache matajiri kuzikalia, kuzihodhi na kurithishana nyumba za NHCkwa miaka mingi.
watu wengi hawajui nini madhumuni ya kuanzisha mashirika kama NHC. BABA WA TAIFA alipokuwa akizungumzia usawa wa binadamu alihusisha mahitaji muhimu ya binadamu kama malazi,mavazi na chakula kwamba kila mtu bila kujali kipato chake anastahili kupata huduma hizo ndio maana shirika la NHC lilianzishwa ili watu waweze kupata huduma hizo kwa bei nafuu na wengine wakiuziwa nyumba kwa bei nafuu. Na hata ubinafsishaji wa mashirika ulipoanza shirika la NHC liliachwa kwa makusudi kwasababu huduma yake bado ilikuwa bado inahitajika kwa jamii.

Nimuhimu kuwe na term limit katika ukazi katika nyumba za NHC. Nyumba hizi ni mali ya umma na zinatakiwa kuwafaidisha watanzania wengi kama sio wote kwa namna moja ama nyingine. Lakini kwa bahati mbaya nyumba hizi zimekuwa zinakaliwa na wapangaji haohao kwa zaidi ya miaka 20 sasa – tena wengi wao wakiwa ni watanzania wenye asili ya kiasia wenye uwezo mkubwa. Kuna watoto wamezaliwa kwenye nyumba hizi na kuolewa wakiwa humo humo. Nadhani hali hiii napotosha malengo ya uanzishwaji wa nyumba hizi. Ninaamini shirika hili lilianzishwa ili kuwapa unafuu wa makazi watanzania wa hali ya chini na kati nasio hawa matajiri wanaozikalia na kuzihodhi sasa. Ili lengo la kuanzishwa kwa shirika hili litimie ninapendekeza mbadili sera ya ukaaazi ili kuwe na term limit katika ukaazi. Upangaji wa nyumba hizi uwe ni wa miaka minne tu na wapangaji wapya wawe ni watanzania wenye umri usiozidi miaka 50. Hii itasaidia kuwapa watanzania wengi fursa yaku enjoy nafasi ya kuishi kwenye nyumba hizi zenye kodi nafuu, na kuishi kwenye mazingira mazuri zilizoko nyumba hizi kwa muda wa miaka minne huku wakijiandaa kuhamia kwenye makazi yao wenyewe au makazi mengine na kuwapisha watanzania wengine ku enjoy fursa ya kuishi katika makazi haya mazuri. Age limit ni muhimu kwani vijana wanaoanza maisha ndio watu wanaohitaji msaada zaidi katika suala la makazi na sio wazee waliokwisha kujijenga (hawa wawaachie watoto wao nyumba hizi za bei nafuu).

Mbili: Uajiri wa Meneja mkuu na makaimu wake na Upimaji wa utendaji wao uangaliwe upya. Meneja mkuu na makaimu mameneja wa shirika hili wawe wanaajiriwa na kamati ya bunge na kila mwaka wawe wanafanyiwa tathmini (performance evaluation) na kamati hiyo ili wasipofikia malengo waachishwe kazi ili tuweze kupata mtu atakae liendesha kwa ustadi mkubwa. Thathmini hiyo igawanyike into financial performance evaluation, Quality of service performance evaluation, Results performance evaluation (kama wamefikia malengona kwa asilimia gani) na customers and non customers survey. Ni muhimu kila meneja apewe targets anazo takiwa kufikia na meneja yoyote atakaeshindwa ku meet 80% ya hizo targets atupishe ili tuweke meneja mwengine mwenye uwezo. Shirika hili ni taasisi ya kibiashara ya serikali – kuna haja ya kuhakikisha kuwa ina fanyabiashara kwa ufanisi na kwa faida – Mameneja wasioeweza kutimiza malengo haya ni vyema wakapisha watanzania wengine wenye uwezo wa kutumiza malengo haya.Mameneja hawa wanalipwa mishahara inayofanana na mameneja wa successful private companies lakini mafanikio yao sio kama ya successful private companies – hapa hakuna uwiano wa matokeo ya kazi (Results) na malipo.

Maoni ya Mdau Zinjathropus
Njia moja ya kutaka kujua mafanikio, mwelekeo mpya wa shirika na quality za service zake ni kupitia feedback from your existing customers. Right now over90% of existing customers with residential tenants agreement are not happy at all with Mchechu's management.

Ukisoma business plan yao walioisoma bungeni ni ujinga mtupu, admittedly on the surface it appears the management wishes to grow and has ambitions of fulfilling the needs of a variety of their potential customers also luring first buyers into their firm.

Anza sasa kufuatilia implemention zao ndio utaona huyu jamaa ni mwendawazimu and has mistaken a public organization for a private one. Kikubwa hasa ni kutokana na background ya Mchechu as a financier where every opportunity must be seized. Despite all their existing scattered unused plots management inaona bora kuvunja some areas that have high returns and remove the existing tenants. Hilo ni shirika ambalo linaona bora kuvunja nyumba ishirini na kujenga mia moja kwa sababu ya return hata kama sehemu zenyewe ipo congested na haina enough infrastructure to accommodate the new population.

Contrary to their existing purposes most of their projects aim at the high end of the market, sasa unajiuliza mfanyakazi wa kawaida kwenye administration ya serikali (civil servants) and low level paid skilled workers such as teachers, nurses, government accountants, police officers etc wataweza kweli kumudu rent zao au kununua nyumba zao? Shirika limekazana na sehemu ambazo zina high returns, wakati wana enough assets to grow organically and still make profit.

Kingine embu fuatilia their finances and the way they raise them halafu uone those obligations zitawachukua muda gani kulirudisha hili shirika katika malengo yaku serv people with lower income, angalia sera zao za partnerships, angalia contracts za benki wanazoingia nao na lenders ni mteja gani hayo mabenki yapo tayari kuwapa mikopo kutokana na interest zao. Mchechu is not fit for the organisation.

Wala usitake nikueleze consumer remedies ambazo zipo pending kwa kuvunja mikataba na kuanza kuwatoza watu kodi mpya ni kesi za ushindi mia kwa mia labda kama serikali aitamkingia kifua zikienda mahakamani (kama unaelewa mkataba unalindwa vipi kisheria). NHC washukuru wapangaji wengi kwa sasa hawaliangalii hilo. Mwisho wa siku NHC watajikuta wanatakiwa kulipa mabillioni ya hela ambazo wame wabadilishia watu mikataba ambayo ilikuwa ya miaka mitano na kuwa lazimishia mipya baada ya miaka miwili kisa body imebadilika trust me si yeye tu kilaza humo ndani bali team nzima ni ovyo.

Halafu eti Dr. Dau huyu jamaa aliejenga machinga complex likadorora, tells you the quality of their marketing teams in those organizations ukiona sasa demands zao kwenye vacancy adverts awe na masters, awe na experience ya senior position isiyopungua miaka kadhaa, halafu hawa ndio watu wanaokuja na upuuzi huo, amazing.
Maoni ya Mdau Fisi 2 -: aise wewe una akili sana. Nimemaliza performance measurement ya Nhc. My first recommendation ni shirika livunjwe haraka. Kuna money laundering kubwa sana Nhc. Najua ni ngumu kupokeleka na kukubali ukweli huu.

Tatu: Mishahara ya mameneja na wafanyakazi itazamwe upya. Hili ni shirika la umma na wala sio a successful private organization. Hakuna haja ya kuwalipa mameneja wake mishahara inayofanana na ile ya a successful private organization. Kuna haja ya kuitizama upya mishahara ya watumishi wa shirika hili ili iwe na uwiano fulani na wafanyakazi wengine wa umma na pia uwe nauwiano na mafanikio ya shirika hasa ukizingatia kuwa ufanisi wa kazi na matokeo ya utandeji wao ni hafifu – hawafikii malengo.
Maoni ya mdau fikirikwanza
Shirika la nyumba la bwana Nehemia Mchechu limekuwa hasara kubwa kwa taifa, kwa maana ukitoa mishahara yao shirika halina mchango wowote kwa wananchi ambao kimsingi walichukua fedha zao kulianzisha, ni shirika ambalo lilipaswa kuwa linatoa gawio kwa wananchi kwa kujenga vituo vya afya, shule au maabara kila mwaka kama faida kwa watanzania kwa kuwekeza ktk kuanzishwa kwa shirika hilo.

Kwa hali livyo sasa ni pesa ya watanzania wote imechukuliwa kuwapa kipato wachache ambao wanafanyakazi NHC kwa faida ya familia zao binafsi, hakuina faida kwa mwekezaji ambaye ni mwananchi kupitia kodi zake kwa serikali. Je ni sahhi taifa liwape biashara watu wachache ambao ndio wanakula kwa njia ya mishahara mapato ya NHC bila gawio kwa wananchi? Nehemia, tumekupa ulaji bila kutulipa kama taifa faida ya aina yoyote? Je kunafaida gani kwa umma kuwa na NHC Tanzania?


Maoni ya mdau fikirikwanza

1 comment:

kolochatechee said...

hodi ni wewe katika haraka haja mkopo kulipia kuanza yako madeni ya kuanzisha biashara au nyumba ??? Kisha inakuja teksi kampuni una imani na relay juu ya 100% uhakika sababu hii ni kampuni ambapo i cashed mkopo wangu kwa mama yangu Stella dawa leo ili kuwasiliana na René Mikopo Firm halisi kupimwa na kuaminiwa na leo mimi nina furaha i got mkopo wangu wa $ 120,000 leo ili kupata kushikamana leo {mrsstellareneloanfirm@hotmail.com} barua pepe hapa chini na kupata jibu la matatizo yako yote kwa sababu Siwezi Kunyamaza ushuhuda huu mkubwa peke yangu binafsi ili i aliamua kuandika kwenye tovuti kwa sababu kula furaha kubwa kwa yangu moyo na leo mimi nina kuishi maisha mapya shukrani kwa wote Stella René


kolochatechee