KLABU ya
Manchester City imepata pigo baada ya kufahamika kuwa huenda kiungo wake
mahiri Yaya Toure asicheze tena msimu huu baada ya kuumia katika mchezo
dhidi ya Liverpool uliochezwa mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa
Anfield.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alitolewa nje wakati wa kipindi kwanza
na kusababisha hali kuwa mbaya kwa kikosi chake na kupelekea kufungwa
mabao 3-2 na mahasimu wao hao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu.
Akihojiwa
kuhusiana na hali ya nyota huyo, kocha wa City Manuel Pellegrini
amesema itakuwa ngumu kwa mchezaji huyo kumaliza msimu huu.
Toure
alijiumiza mwenyewe baada ya kupiga shuti lililopaa katika mchezo huo
wakati City wakijaribu kurejea baada ya kufungwa bao la kuongoza na
Raheem Sterling
No comments:
Post a Comment