Mike Lukindo enzi ya uhai wake.
Suala ninalotaka kulizungumza leo, ambalo limeugusa moyo wangu, yaani limeniumiza sana kwa kilichotokea kwa marehemu Lukindo, sio utamaduni wetu sisi Waafrika kuchomwa moto, la hasha
, huwa tunazikwa kwa heshima na upendo.
Ni kweli maisha yetu si ya kitajiri kwenye hizi nchi za watu, vipato vyetu havituwezeshi kuweka akiba sana,ikizingatiwa pia tuna familia nyumbani ambazo zinatutegemea.
Ninaomba sana, pamoja na majukumu tuliyo nayo, tujitahidi kulipia NSSF WESTADI dola 300 tu kwa mwaka ili ikitokea bahati mbaya mmoja wetu amefariki, tushiriki kuifariji familia,bila kuumiza
kichwa kuhusu michango.
Tunamshukuru sana sana Muheshimiwa Balozi wetu Mama Mulamula, kwa kutusaidia kwa namna
moja au nyingine kufanikisha usafirishaji wa Miili ya wapendwa wetu., sasa inabidi tujitume,tuwe na
hiyo Bima Ya NSSF ambayo ni hela kidogo sana.
MDAU U.S.A

7 comments:
Kwa nini tusizikwe hapahapa? why bother with NSSF?
Kwani ukipelekwa kwenu nini kinabadilika? Unajua huu uwezo wetu wa kufikiria umefika ukomo, yaani unakuja na idea hapa kwamba we need to invest 300 kwa mwaka ili kupelekwa nyumbani tukifa?
Asante sana kwa ushauri mzuri. Watanzania inabidi tuamke na kutumia marupurupu mbali mbali tunayotangaziwa.
Hivi unafikiri kuwa mwili wake umechomwa sababu ya kukosa pesa? Hivi unajua kuchomwa pia ni maamuzi ya mtu kabla hajafariki? Unajua kuwa nyumbani pia watu wanachomwa?
Sina na siuamiini mfuko wa NSSF, sio kwamba sina pesa bali mfuko huohuo unakopwa na wannasiasa. It is a matter of time kabla hatujasikia um
e-kauka. Nimuhimu kuwa na life insurance au akiba maalum kwaajili
itakayosaidia maaziko yako lakini sio through NSSF. In long run NSSF haiiwezi survive labda ibadili uendeshaji.
Ni vizuri watu waweke wosia wao mapema ili ikitokea siku wamekufa ijulikane kabisa kama kuchomwa hapa marekani au kuzikwa nyumbani HII ITASAIDIA SANA KUONDOA USUMBUFU...
Nyote hapo juu hamna akili, la muhimu lilikua ni kuchangisha pesa ili mwenzetu aliyetuacha asafirishwe na kuzikwa kwa amani nyumbani Tanzania. Hizo comments hazina faida, tumewachangia wengi waliotutoka, hivyo basi tusikate tamaa ya kuendelea kufanya hivyo. Huo ndiyo uzalendo wadau.
Mpango wa WESTADI sio tu ni kusafirisha mwili nyumbani bali hata kuzikwa au kuchomwa hapa nchini ambavyo vyote ni gharama. Kutokana na kifo cha Bw. Lukindo nimegundua kuwa gharama ya kuzika hapa nayo siyo ndogo, ilikuwa USD 6,000 wakati ya kuchoma ilikuwa 2,000. Life insurance ya Marekani process yake ni nzuri pia lakini process yake ni ndefu sana kuweza kukusaidia kwenye maziko. Zaidi ni kusaidia familia unayoiacha nyuma. Natumaini ufafanuzi huu utasaidia kwa wale ambao hawaoni umuhimu wa WESTADI. Siamini kwamba NSSF itafilisika leo au kesho. Anyway mtaalam wa WESTADI atakujkutuekezea zaidi kuhusu mpango huu wakati wa maaadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wetu. Msikose fursa hiyo ili muweze kutoa dukuduku zenu zote. Mbarikiwe wote!
Post a Comment