Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kuhusu Ajali ya Ndege ya JWTZ aina ya Helikopta katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyokuwa imewabeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dr. Ghalib Bilal na ujumbe wake ambao ni Waziri wa Ujenzi; Mhe. Dr. John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Said Mecky Sadick na amishina Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Kamishina Suleiman Kova.
Helikopta hiyo ilikuwa imewabeba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dr. Ghalib Bilal na ujumbe wake ambao ni Waziri wa Ujenzi; Mhe. Dr. John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Said Mecky Sadick na kamishina Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Kamishina Suleiman Kova.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na wananchi wote kwa ujumla kuwa jana tarehe 13 April 2014 mnamo saa tatu na nusu asubuhi (3:30 Hrs), kumetokea ajali ya Ndege ya JWTZ aina ya Helikopta katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere ( upande wa Jeshi). Helikopta hiyo ilipata ajali ilipokuwa katika hatua ya kuanza kuruka.
Aidha, Wengine waliokuwemo ni Dr. Mnzava, Msaidizi wa Makamu wa Rais, Msaidizi wa Kamanda Kova na waandishi wa habari watatu.
Ujumbe wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa katika safari ya kuzungukia maeneo yaliyo athirika na mafuriko katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kufuatia mvua kubwa iliyoanza kunyesha kuanzia tarehe 11 April hadi sasa.
Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wake hawakupata majeraha katika ajali hiyo. Aidha, rubani na wasaidizi wake pia wametoka salama.
Uchunguzi wa ajali umeanza mara moja kwa ajili ya kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0754270136
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
1 comment:
Naona kama kuna vitu vingi hapa vipo kienyeji kienyeji. Kwanza hii habari imerudia rudia kuwataja wahusika wa ajali kitu ambacho siyo muhimu. Pili mtoa taarifa amesema saa tatu na nusu halafu akaweka kwenye mabano saa za jeshi kama 3:30 hours. Kwa usahihi saa 3:30 za kiswahili zinatafsirika kama 0930 hrs. Tatu, aliyetoa taarifa ameandika simu yake ya cellphone badala ya landline, kitengo kikubwa au idara kama ya serikali tulitarajia kuona namba ya simu ya mezani. Tunahitaji jeshi la wasomi.
Post a Comment