Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu (FRAT) Mkoa wa
Singida, Josephat Magazi kilichotokea jana mkoani Kilimanjaro.
Magazi
ambaye pia aliwahi kuwa mwamuzi na kamishna wa mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) alikuwa amelazwa katika
Hospitali ya KCMC. Mazishi yatafanyika kesho (Aprili 15 mwaka huu) saa 5
asubuhi kwao Ushirombo mkoani Shinyanga.
Msiba
huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti
Magazi alishirikiana na TFF na wadau wengine wa mpira wa miguu katika
masuala ya uamuzi na uongozi, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Magazi, FRAT na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Singida (SHIREFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
No comments:
Post a Comment