Friday, January 2, 2015

MBUNGE WA MOROGORO MJINI ATOA WIKI MBILI KWA MTENDAJI WA KATA KURUDISHA FEDHA ZA WANANCHI

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza kwa makini Kero Mbalimbali zinazowasumbua wakazi wa kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro sambamba akiwa na Diwani wa Kata hiyo kushoto Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lugala Kulia.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea Taarifa za Maendeleo kata ya Luhungo Kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa Kata Hiyo
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwasikiliza viongozi wa Watendaji wa kata ya Luhungo Iliyoo Manispaa ya Morogoro mara baada ya Kukagua eneo la Ujenzi wa Shule ya Awali Ambapo Mh Mbunge Amechangia Jumla ya Shilingi Milioni 2
Wakazi wa Kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro waliojitokeza Kumsikiliza Mbunge wao Mh Abood aliowatembelea Kusikiliza Kero zao Ambapo wakazi hao walilamikia Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata hiyo Mzee Makame Kai aliyefuja Fedha za Miradi ya Maendeleo Pamoja na Kuuza pembejeo za wakulima.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea Taarifa za Chama Kutoka kwa Katimu wa CCM Kata ya Luhungo
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Kivuko Kinachounganisaha Mtaa wa Majengo na Mshikamano Eneo la Lukobe Kata Ya Kihonda Manispaa ya Morogoro wakati wa Mfululizo wa Ziara zake ya Kutembelea Kata Zinazounda Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Mbunge aliahidi Kujenga Kivuko Hicho mara baada ya Kutembelea Eneo Hilo na Ndipo wakazi wa Eneo hilo walipomwomba Mbunge wao Kuwatatulia Kero ya eneo hilo muhimu inayowaunganisha wakazi wa Mitaa hiyo
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Ujenzi wa Kivuko hicho ambapo Mpaka ujenzi utakapokamilika Utagarimu jumla ya Shilingi Million 6.

No comments: