Treni mpya ya kisasa ya Deluxe jana imeanza safari zake kutoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Meneja Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez, alisema safari hii ni ya pili tangu treni hiyo izinduliwe Aprili Mosi mwaka huu ambapo ilikwenda Kigoma.
“Safari za Delux zitakuwa kwa wiki mara moja, siku ya Jumapili itaondoka stesheni ya Dar es Salaam saa 2:00 usiku ikiwa na mabehewa 15.
“Treni hiyo itakuwa na madaraja matatu ambapo daraja la kawaida litakuwa na mabehewa 10 na kila behewa moja litakuwa na abiria 80.
“Daraja la pili litakuwa na mabehewa matatu ambalo ni la kukaa, kila behewa moja litakuwa na abiria 60 na daraja la tatu la kulala litakuwa na mabehewa mawili ambapo kila moja litakuwa na abiria 36.
“Treni hiyo itasimama katika vituo 17 ambavyo ni Morogoro, Kilosa, Dodoma, Makutopora, Saranda, Manyoni, Aghondi, Itigi, Tabora, Urambo, Kaliua, Uvinza na Kigoma.
“Vituo vingine ni Isaka, Shinyanga, Malampaka na Mwanza ambapo wiki moja itaenda Kigoma na wiki inayofuatia itaenda Mwanza,” alisema Maez.
Alisema treni hiyo ni tofauti na zinazotumika sasa kwani ni ya kisasa na ina huduma mbalimbali muhimu ambazo ni sehemu za umeme kwa ajili ya kutumia vifaa vya kisasa kama kompyuta mpakato, simu za mkononi na mtandao wa intaneti.
Maez alisema treni hiyo pia ina vyoo vya kisasa ambapo katika kila behewa atakuwapo mtaalamu wa kutoa elimu kwa abiria namna ya kuvitumia.
Alisema wasafiri wa Dodoma na Tabora watapata fursa ya kutumia usafiri huo wakati wote isipokuwa wale wanaoishia Kigoma na Mwanza na mabehewa mengine ya Delux yatakapopatikana safari zitakuwa kila wiki kwenda Kigoma na Mwanza.
“Lakini ipo tabia kwa baadhi ya wananchi kuharibu au kuiba mali za reli, vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwa hiyo nawaomba washirikiane nasi katika kulinda miundombinu ya reli ili tuweze kutoa huduma kwa miaka mingi ijayo,” alisema.
Nauli zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma daraja la kawaida ni Sh 35,700 daraja la pili Sh 47,600 na daraja la kwanza Sh 79,400.
Aidha nauli kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza ni Sh 35,00 kwa daraja la kawaida, daraja la pili Sh 46,700 na daraja la kwanza Sh 77,800.
Mpekuzi blog
9 comments:
Huu unene .ni ugonjwa .mwenyewe ,anasema pesa. ni shidaaa.
Hili jina lake vipi? walikoseaga? Midladyj?
Ni sheedaahh
Ni sheedaahh
Badae xana
Ikitoka io saa mbili usiku inafika saa ngapi toka dar to mwanza
Ikitoka io saa mbili usiku inafika saa ngapi toka dar to mwanza
Ikitoka io saa mbili usiku inafika saa ngapi toka dar to mwanza
Ikitoka io saa mbili usiku inafika saa ngapi toka dar to mwanza
Post a Comment