Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard akitoa elimu ya afya kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Msimbazi Mseto.
Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard leo amekabidhi msaada pamoja na kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike katika shule ya msingi Msimbazi Mseto.
Huu ukiwa ni mwendelezo wake katika kufanya kazi za kijamii, Caroline ambaye ndiye aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania 2014 ataendelea kulitumikia taji lake kama mrembo mtawazwa ingawa alishindwa kwenda kushindana kimataifa kutokana na sababu za kiafya.
Caroline alishindwa kwenda kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa2014 na badala yake kwenda mshindi wa pili Nale Boniface mara baada ya kuumia kidole cha mguu wiki chache
kabla ya mashindano.
Mpaka atakapokabidhi taji baaadae mwaka huu, Caroline ndo ataendelea na taji lake ndiye atakayemvisha mtaji mshindi wa 2015. Msaada alioutoa caroline ni pamoja na vitaulo vya kinamama (hygiene pads) vya kujihifadhia wakati wa hedhi na karatasi ya kujisafishia maarufu kama tissue.
“Nimelenga kushughulika na watoto wa kike hasa wa shule ya msingi darasa la sita na la saba kwani hawa ndio wanaotakiwa kujitambua zaidi hususani mabadiliko yao ya kimwili huanzia hapa.”Alisema mrembo Caroline.
Miss Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake alikuwa Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi yetu ya Tanzania kwa kushika nafasi ya Sita kidunia.Mwaka uliofuata, 2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi Flaviana Matata na kuvaa taji la Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata James mwaka 2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010.
Baadae taji lilichukuliwa na Nelly Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo Winfrida Dominic. Mwaka 2013 taji lilienda kwa mrembo Betty Boniface na hatimaye kumuachia mikoba mrembo Caroline Bernard Miss Universe 2014.
No comments:
Post a Comment