Wednesday, August 19, 2015

MASHABIKI WA LOWASSA, MUMEYAFIKIRIA HAYA?

Picha kwa hisani ya Michuzi
Na Mwandishi wetu

NAOMBA nikiri kwamba pamoja na kuwa mfuatiliaji sana wa mambo ya siasa, nchini na duniani kwa ujumla, si kawaida yangu kuandika hasa kuhusu siasa kwenye magazeti. Nimeaamua kuvunja kawaida yangu baada ya kuona mushkeli mkubwa kuhusu namna ambavyo siasa zetu zinakwenda katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.
Liko vuguvugu kubwa limezaliwa sasa nchini, wananchi wengi wanasikika wakitaka mabadiliko, hii ni haki kabisa kwa sababu chini ya jua hakuna kitu cha kudumu isipokuwa mabadiliko. Hiyo kiu ya mabadiliko ni haja ya kawaida kabisa kwa binadamu yeyote.
Lakini kitu kinachonitisha kuhusu mabadiliko ya wanayoyatamani baadhi ya Watanzania, ni aina ya mabadiliko wanayoyataka, na mtu wanayeamini ataleta mabadiliko hayo.
Aliyekuwa mtia nia wa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, ambaye sasa ni mgombea wa Urais kupitia Chadema, akiungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ndiye anayeonekana kuwa mbeba bendera ya mabadiliko hayo. Sina tatizo binafsi na Lowassa, lakini kinachonitatizo ni vitendo vyake kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Najiuliza ni kwa kiasi gani wafuasi wa Lowassa, walioko Chadema na Ukawa na wale wanaomfuata alikohamia kutoka CCM, wanachukua hata dakika moja kutafakari aina ya mtu wanayemuunga mkono kwa nguvu zote namna hiyo. Hayo mabadiliko wanayoyaimba kila siku yataletwa naye wanajua ni mbadiliko ya aina gani?
Sitaki kuwahukumu, lakini sina uhakika kama wanatafakari kwa makini aina ya mabadiliko wanayotaka na mtu wanayemtumaini kuongoza mabadiliko hayo.
Dalili zinaonyesha uko uwezekano mkubwa wanafanya hivyo kwa sababu wameamua kuwa mashabiki tu ili kuridhisha nafsi zao.
Duniani kote viongozi wanaoongoza mabadiliko au mapinduzi yaliyoleta manufaa kwa jamii zao, kwanza ni lazima wawe na falsafa wanayoisimamia, wawe tayari kuifikia falsafa hiyo, na zaidi sana wawe na msimamo unaoaminiki, kiasi kwamba yeyote anayemfuata anakuwa na uhakika na kauli na vitendo vya kiongozi huyo.
Kuwa na kigeugeu haijawahi kuwa sifa ya kiongozi wa dhati anayesimamia mabadiliko ya kweli kwenye jamii.
Nikimtazama Lowassa, kwa dhati ya moyo wangu, sioni kama ni kiongozi wa kuaminika, sioni ndani yake uongozi wenye uwezo wa kusimamia kauli zake kwa dhati, bila kujali zinaweza kumgharimu kiasi gani ili mradi anaamini katika msingi ya aina fulani. Siyasemi haya kwa sababu nina chuki binafsi naye, lakini nayasema kwa sababu ni mambo yaliyo dhahiri kwa kila mtu.
Mei 30, mwaka huu 2015, wakati anatangaza nia kuomba kuwania urais kupitia CCM, jijini Arusha haya ndiyo aliyotuambia Watanzania.
“Kiuchumi, tumeshuhudia ukuaji mzuri na kuongezeka kwa mapato ya ndani ya Serikali na uimarishaji wa mfumo wa uwajibikaji na ulipaji kodi. Kwa upande mwingine, Serikali ya Rais Benjamini Mkapa na Rais Jakaya Kikwete zimefanya kazi kubwa katika uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi asilia ambapo kiwango kikubwa cha gesi asilia kimegunduliwa.
“Tanzania sasa imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazovutia uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo ambayo inatajwa kwamba inaweza kuja kubadilisha kabisa maisha ya Watanzania.
“Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kipindi chake na kama ambavyo amekuwa akisisitiza mara kwa mara katika hotuba zake za karibuni ni kwamba yeye ametekeleza wajibu wake.
“Pia amesema anamwachia atakayemkabidhi uongozi wa nchi yetu baada ya yeye kumaliza muda wake kuendeleza pale atakapoachia”.
“Serikali za awamu zilizotangulia zimeyajadili na kujaribu kuyatafutia ufumbuzi. Mimi pia nimekuwa sehemu ya jitihada hizi wakati wa utumishi wangu katika chama na serikali huko nyuma”.
Ilipofika Agosti 10, mwaka huu 2015, baada ya kuchukua fomu ya uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, alituambia Watanzania kwamba;
“Rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete kauharibu uchumi wa nchi, lakini sitaki kutoa mashtaka nataka kuzungumza kwa data, mwaka 2005 wakati Rais Benjamin Mkapa alipomaliza muda wake kilo moja ya sukari ilikuwa shilingi 650 lakini sasa hivi kilo moja ni Sh. 2,300, mchele umepanda hadi Sh. 2,220, sembe ni Sh. 1,200 na kibiriti ilikuwa Sh. 50 lakini sasa hivi ni Sh 200,”
“Katika hali hiyo CCM haina haki ya kuendelea kutuongoza, nawaalika wenzangu waliobaki CCM waje bila haya, waelewe matumaini yapo ndani ya chama chetu, (Chadema)”.
Lakini akitangaza nia Arusha huu ndiyo ulikuwa msimamo wake kuhusu CCM;
“Najua kwamba Ilani ya CCM ya mwaka 2015 imo katika hatua za mwisho za kukamilishwa na itakapopata baraka za vikao vya chama itakuwa ndiyo msingi wa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano itakayochaguliwa Oktoba mwaka huu.” Hapo alikuwa akimaanisha serikali itakayoongozwa na CCM, lakini akaongeza
“Lakini kama alivyotuusia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1995, wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini, Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM!
“Sina shaka, CCM tunao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka”.
Wiki chache baadaye msimamo wake ukawa huu; “Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kujidanganya mimi mwenyewe na umma wa Watanzania kwa kusema kuwa bado nina imani na CCM au kuwa CCM ni chama kitakachowaletea ukombozi wa kweli wa kiuchumi, kisiasa na kijamii. CCM niliyoiona Dodoma siyo tena kile chama nilichokulia na kilichonipa malezi na maadili ya siasa yaliyojengwa kwenye misingi ya haki, usawa na uadilifu.”
“Ni dhahiri kwamba CCM imepotoka na kupoteza mwelekeo na sifa ya kuendelea kuiongoza Tanzania yetu. Mimi kama Mtanzania aliye na uchungu na nchi yake nasema imetosha na sasa basi!
“Hivyo basi, baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kuwa kuanzia leo ninaondoka CCM na kuitikia wito wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya kweli ya nchi yetu”.
Ukiyasoma kwa umakini maneno haya, unaona wazi kwamba ndani ya kipindi cha majuma nane, amekuwa na misimamo miwili mizito inayokinzana kuhusu CCM.
Ninachokiamini mimi ni ukweli kwamba CCM inaweza kuwa na matatizo yake makubwa, lakini haiwezekani yakawa yalitokea ndani ya muda mfupi kiasi hicho, yaani kuanzia alipokatwa, na alipohamia Chadema. Kama kupoteza mwelekeo wa kuongoza hakuwezi kuwa kumekuja CCM ndani ya muda wa siku 30 tu, kama huo ubovu upo aliuujua tangu kabala ya kuchukua fomu kugombea Urais.
Sasa kama alitambua hilo, kwanini aliamua kuimwagia sifa CCM na uwezo wa ilani yake kuingoza serikali ya awamu ya tano, lakini alipokatwa ghafla zile sifa ‘nzuri’ za CCM zikafutika. Mara ghafla ikawa hakiwezi tena kuingoza nchi, msimamo ambao unakinzana na kauli yake aliyoitoa siku chache zilizotangulia.
Katika hili ni ama akiwa CCM alitudanganya ili apate anachokitafuta, au alisema ukweli na sasa akiwa Chadema, anatudanganya ili apate anachokitafuta, au anasema ukweli lakini awali alidanganya. Vyovyote vile inavyoweza kuwa, ndani ya muda huo wa kuhama kwake, kuna mahali amewahadaa na kuwadanganya Watanzania.
Hapa ndipo ninapopata shida, kwa sababu mtu ambaye kwa muda mfupi namna ile amekuwa na misimamo miwili tofauti inayokinzana kisiasa, unawezaje kumuamini kwamba hiki anachokisema sasa ni kweli na siyo uongo kama ambavyo alituambia Mei na anayotuambia sasa.
Sina uwezo wala mamlaka ya kumchagulia mtu aina ya mtu au chama cha kuunga mkono kwenye siasa, hilo litakuwa ni kuingilia uhuru wa mtu, lakini ninao wajibu kama raia mwema wa taifa hili, kuwakumbusha wananchi kuona kile ambacho inawezekana wengine hawakioni au hawataki kukiona.
Tunapotaka mabadiliko lazima pia tuukubali ukweli mchungu kwamba mabadiliko lazima yawe ni kwa manufaa mapana ya jamii yote, na siyo ya kikundi cha watu wachache, kuwatumia wananchi wengi kujipatia maslahi yao binafsi.
Mabadiliko yoyote yale lazima yasimamiwe na watu makini, wanaoweza kuaminika, kutumainiwa kutokana na uthabiti wa maneno ya vitendo vyao, umuazi wa kuwa na misimamo miwili inayotofautina mithili ya mbingu na ardhi ndani ya muda mfupi hivyo kwenye mambo makubwa ya nchi, haiwezi kuwa sifa ya kutumainiwa kuongoza mabadiliko tena.
Mwandishi wa Makala haya, amejitambulisa kuwa ni Juma Khalfani mtumishi mstaafu wa serikali na msomaji wa gazeti hili anayeishi Shinyanga.

RAIA MWEMA

19 comments:

Anonymous said...

Nashukuru sana kwa maoni yako. Watu tunataka mabadiliko. Nchi zote zilizoendelea ufaya mabadiliko. kuna ubaya gani chama kingine kijaribu miaka 5 au miaka 10. Jamani acheni kuogopesha watu, mtoto akililia wembe mpe!!
ahsante sana.
Jimmy.

James Bond said...

Tumechoshwa na CCM. .CCM si baba wala mama yetu....kama ikibidi tuitoe kwa mkono wa Lowassa basi tutaitoa..kila mTanzania aliezaliwa miaka ya 1961 mpaka 1990 hakukuwa na uchaguzi wa Chama zaidi ya CCCM KWA man tiki hiyo ni kuwa karibu ya robo tatu ya Wa Tanzania walishawahi kuwa wa na CCM sasa kama wewe una matatizo na Lowasa hilo ni lako..sisi tunakwenda kuitoa CCM mwezi October. .history iko na sisi..CCM imezeeka na kamwe haitotolewa na mtu wa nje ya CCM ni mtu kutoka ndani ya CCM ndiyo kifo cha CCM. .wewe subiri kufa kwa kuwa mabadiliko kwako ni shida

Unknown said...

So hoja yako hasa nini? Nimeshindwa kukuelewa na hueleweki, lipi jipya kwani

Anonymous said...

Very well said! Excellent conclusion!

Watu wanashabikia tuu bila kutafakari mara mbili mbili wanajitia upofu hawajui wanaliangamiza taifa na watakao umia ni mama zetu na watoto.

Ndio tumeichoka CCM lakini je hawa tunao taka kuwapa ni Mbwa Mwitu walio vaa ngozi ya Kondoo!!!

Anonymous said...

Wewe hata ukiandika vitabu milioni ya tahadhari kuhusu kuchagua upinzani pamoja na uzuri wa ccm, hiyo haitasaidia kitu my friend. Watu wanataka mabadiliko. Watanzania wengi wako tayari kumpigia mbwa kura but not ccm. So hapo unajisumbua na kupoteza muda wako kuandika tahadhari. Tahadhari gani. Why don't you write facts about ccm kushindwa kuwasaidia wananchi wa kawaida?? Shule vijijini nyingi tu bado hazina majengo mazuri na vifaa bora vya kusomea watoto. Hosipitali nyingi hazina madawa wala njia bora za kutibia wagonjwa. Watu wenye uwezo wanakwenda kutibiwa nje including Kikwete mwenyewe miezi iliyopita alikuja kutibiwa huku US. Vipi kwa mwananchi wa kawaida asiyekuwa na uwezo wa kwenda kutibiwa nje, atafanya nini zaidi ya kusibiri kufa. Watu wengi hawana kazi pamoja na kuwa na elimu. Rushwa na ufisadi chini ya ccm ni mtindo mmoja. Well, vipi the so called miundo mbinu?? Barabara zinajengwa kama vichochoro by spending so much money for minor things instead of bigger things. The list goes on and on. Kwa miaka zaidi ya 50 maendeleo chini ya serikali ya ccm yako machache sana kiasi ya kutowaridhisha wananchi wa kawaida. Watu wamechoka na ccm. Yaani wamechoka sana, I am telling you my friend. Wageni wanaogopa kuja kuwekeza huko kwa kuogopa corruption kubwa chini ya serikali ya ccm. Sio kwamba upinzani wakishinda wataweza kuleta maendeleo overnight la hasha, it's a process. Sasa hivi Watanzania do not care other than too see ccm's gone.

Anonymous said...

Hivi Lowassa kawakosea nini CCM
Kumtukana hivi
Lakini mjuwe Lowassa in chagua letu mwaka mtaula na chuya

Anonymous said...

Nampongeza Muandishi Khalfan,kwa kuandika maelezo ambayo yanaweza kukuvutia kuyasoma kwa kuwa amejaribu kuandika kwa kuweka substances. Reference quotations.
Ila ninadhani Khalfani inawezekana hataki kukubali au hajui kama Mheshimiwa EL alikuwa na mikakati ya kuingiza mabadiliko chanya ya ki mfumo ndani ya CCM na hatimae Serikali yake ambayo alikuwa anamtazamo wa kuja kuongoza.
Sasa, binafsi sioni dhambi yoyote kwa EL kusema alichosema akiwa ndani ya CCM, Kwa kuwa huo ndo ulikuwa mtazamo wa CCM na yeye alikuwa akitoa vision yake.
Khalfan na wengine wote wanaosumbuliwa na Jinamizi la EL kutoka CCM na kuingia kambi ya upande wa pili, ni kuwa EL kama mtu alikuwa na uhuru wa kuchagua kitu chochote anachotaka, chama, siasa, dini n.k
Napenda walionasa katika butwaa la EL kuondoka CCM waamke, EL yupo upande mwingine sasa hivi, na anafanya mipango thabiti na hatua za makusudi kuingoa serikali ya CCM madarakani akishirikiana na watu waliopo katika upande huo alipo na wanafanya kazi kubwa kuwashawishi wananchi ambao ndio waamuaji kuwaunga mkono katika harakati hizo.
Nadhani Khalfan maandishi yako hayatakuwa na athari yoyote ile kwa harakati za EL na wenzie hivi sasa, na kama unadhani juhudi za EL na washiriki wake hazitakuwa na maslahi mazuri kwako wewe binafsi na kwa taifa basi ungana na kundi la CCM kushawishi wananchi otherwise.
But based on History, EL ana nafasi nzuri ya kukuweka wewe na wengine wote msioamini kinachotokea hivi sasa kwenye deep suprise. He can actually easly win the Election. Na kitakachompa ushindi si ukweli wake au uwezo wake wa kuongoza bali ni fact that CCM na Serikali yake wamekuwa madhalimu kwa wananchi wa kawaida kwa muda mrefu sana, hawakutumia nafasi ya uzoefu wao wa kuongoza kuwasaidia watu bali kuwakandamiza watu, na zaidi Maisha ya mtamzania wa kawaida yameshuka sana kulinganisha na wakati tulio nao.
Mimi ninaishi USA, ilipofika election kati ya McCain v/s Obama, most people whom used to believe on business as usual they gave Obama no chance of succeeding, a lot of negative aspects were brought forward against Obama himself, his convictions, his leadership ability etc. For about 200 years American leaders were elected only white male, Obama as a black men were given no chance, to be honest, I was among those whom believe the men got no shot to stand against white man and I did not vote for him too, not because of his skin color but because I was not believing that he will bring any change into America economy.
Khalfan, with all the odds and nay sayers wishes and prayers, Obama won and became the first African american president in USA. He lead the country for the whole first term, re run and won again. How is or was his performance as president to me is 50/50 (Good and Bad)
So, EL too I bet he will win the Tanzania Election very easy not because of his ability to lead, or what good he will do to Tanzania, his victory will be based on protest that majority of Tanzanian will vote against CCM, but it will not be because they believe on EL.
It is that simple, I wish CCM were to position themselves beter 10 years ago to encounter the rage of Ordinary Citizens, but it did not focus on that, the leaders focused on repositioning their sons and daughters to be future leaders rather that building a good political party that will lead Tanzanians.

Anonymous said...

Nadhani watu wamechoka na chama tawala. Sorry!

Anonymous said...

Lowassa kawakosea nini
Kanyamaza kimya kwenye blog yenu ya CCM mmeweka magazeti yanayomkashifu Lowassa
Lowassa in mchapa kazi si mpiga makerere makukwaani
CCM Kama nafikiri watanzania wanataka wapiga vigembe majukwaani poleni
Ukawa wamejipanga
Kumbukeni
Mmechaguwa watu pro Tibaijuka kugombea ubunge pamoja na rais kumfukuza kazi kwa ajili ya rushwa
Tumechoka Tumechoka
Ukawa karibuni tujaribu mapya

Anonymous said...

Kwa Mimi ninavyoona politics is a bad business , we saw great country like US, UK even Russian leader change their story all the time, is just a politics as usual, The problem here is policies and principal of the leader / political party. CCM have been in power for over 50yrs and we see what we get from their leader and policies , nothing but same all promises for over the yrs, while the ministers and other CCM leader get reacher and reacher over the Tanzanian sweat. Bad contract over and over , corruptions scandal , mis use of government fund and property, un ethical at work with no worry , and final our leader (CCM) are above the law, do whenever and it's ok, no one is punish because we are above the law, CCM is not own Tanzania, Tanzania is property of Tanzania people, it's time to go and may be you will realize what you really miss and opportunity you waste over the yrs to make life better for your own brothers , sister , uncle, parents, and all your fellow friends around Tanzania. When you get sick instead of go over seas for treatment you got to the facility your government build for all Tanzania, your kids go to school in the best school we have in our country instead of ship your kids around the world to get educated, all this is because you all know our school are very insufficient , just like our hospital.time to go CCM. FOOD FOR THOUGHT.

Anonymous said...

Mwizi tu lowassa hafai hata kuwa mlinzi wa shule. Arudi monduli akaendeleze ufugaji wakati akisubiri ukimwi ummalize shwaiiiiiin!!!

Anonymous said...

Unajua nyie Watanzania wa huko Overseas ni so hopeless, mnashindwa kutafakari kwa kina maendeleo ambayo yameletwa na CCM pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili. Habari zenu nyingi ni za kusikia. Wengi wenu hamjafika pale Tanzania kwa muda mrefu, actually tangu mlipotoka pale aidha kwa sababu wengi wenu ile immigration status yenu haiwaruhusu ama wengine hamna nauli za kuwavusha huko. Mkitaka ukweli wa mambo fungeni safari nendeni pale nyumbani mkajionee maendeleo yaliyoletwa na Chama Tawala CCM.

Anonymous said...

Acheni maneno maneno Watanzania wa Overseas. Tafuteni nauli na pesa za uwekezaji ili mkawekeze pale Bongo badala ya kukalia majungu majungu. Na hilo ndilo tatizo kubwa sana kwa Watanzania waliopo nje ya Nchi.... MAJUNGU!!!!!!

Chabicheka said...

Folks here is the problem. Firts we all agreed thaty CCM failed to bring desired change in it's 50 years of ruling walala hoi. Walala hoi are fed up with CCM, and based on comments here it seems that UKAWA could have put anybody agianst cCM and won. So the problem is why oick on someone who just switched ideology in lesss than a month, why not pick someone fresh, young energetic and revolutionary? Are you guys telling m,e that with all this time UKAWA had nobody and wallah, EL landed on their lap. The problem we did was to waste a great opportunity ever happened of not only defeating CCM but also get someone who would have been a game changer and bring real change. To me it seems we are bringing CCM but under the name of UKAWA -same crap. It is not about the party it is about the ideology of who is leading the party -I hope EL wins but then we are going to be marching in the same spot, while we could have brought in real change that walala hoi could benefit. It's a shame.

Anonymous said...

nani kamchagua lowasa??!!, aliyemchagua lowasa ni mbowe na hao vibaraka wake waliopewa mgawao!!! sasa wewe unayesema ni chaguo letu, ni nani hao kina letu???? subiri oktoba muanze kusema tena kura ziliibiwa oooh uchaguzi haukuwa wa haki. chaguo la mbowe haliuziki wala hatuna muda wa kumsafisha. sasa subiri sana

Anonymous said...

Sikio la kufa halisikii dawa. Problem ni the way tunataka kufanya mabadiliko. Mabadiliko mkiwa na watu waliokuwepo CCM tena wakiwa na nafasi za kufanya mabadiliko wakiwa huko CCM na walikuwa na nguvu za kutosha kufanya mabadiliko na hawakufanya mabadiliko:ni ndoto kupata mabadiliko ya kutusaidia Watanzania lather tutabadili tu chama na amini usiamini almaarufu wa CCM (Tunaowaona mafisadi) karibu wote watahamia huko na kuibadili chama kuwa na mambo yaleyale kiCCM. Kama CHADEMA walitaka kutukomboa na ufisadi wa CCM basi hili ni "bao la mkono" mafisadi wamwondoa Silaa ambaye kwa kweli ndio pekee alikuwa na uwezo wa kupambana na mafisadi bila huruma; na kumweka Mtu wao tena kwemye nafasi ya Silaa(Nafananisha ukali wake na Michael Satta, RIP). Lowasa ni wazi akinyosha kidole kutakuwa na vidole vinamtazama sio lazima iwe sababu ni fisadi ila mfumo aliokuwemo ni wazi atakuwa ni sehemu ya maamuzi mengi yakiwemo yenye sura za kifisadi au yenye kuharibu uchumi. Navyoona mafisadi wengi wataendelea kupeta tu na nchi haitabadilika. Mabadiliko ya kweli bado. Tumejaa ushabiki. Tunashindwa kukemea hili bao la mkono. Kwani nani aliwaambia bila kuchukua mtu toka CCM CHADEMA ingeshindwa? Mmeiharibu nguvu ya CHADEMA. Inashindwa kutetea waTanzania badala yake imebaki kusagisha watu na kujisafisha yenyewe.

kanga manyoya said...

ccm mmechoka punzikeni wajameni

Anonymous said...

Mwaka huu wa Lowassa tu hata aje mtu na millioni 10 siuzi kura yangu nitampa Lowassa tu.

kidoo said...

Tena Luna mfumuko Wa kalamu za kubadilisha matokeo wananchi muende vituoni nakalamu zenu