Wednesday, August 19, 2015

RAIS KIKWETE AMTAMBULISHA MGOMBEA URAIS WA CCM KWA WAZEE WA DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, (Watatu kushoto), na viongozi wengine wa ngazi za juu wa chama hicho, kutoka kulia, Katibu Mbuu, Abdulrahman Kinana, mgombea urais wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Dkt. John Pombe Mahufuli, Mwenyekiti wa Wazee wa jiji la Dar es Salaam, Mzee Athumani Mtulia, mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan, na Makamu mwenyekiti wa CCM, (Bara), Philip Magunga, wakifurahia jambo wakati Rais Kikwete, alipomtambulisha mgombea huyo wa CCM kwa wazee wa jiji la Dar es Salaam, hatua iliyoelezwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Kinana, kuwa ni kuomba Baraka kabla ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu
JK akimtambulisha mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan
Dkt. Magufuli akihutubia wazee
Meza Kuu ikimfurahia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam
Rais Kikwete, (kushoto), akiteta jambo na Dkt. Magufuli na katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Mzee Mtulia akisalimiana na Samia na Dkt. Magufuli

7 comments:

Anonymous said...

Swali la kizushi. Ni wazee wa dar au wa ccm?

Anonymous said...

njaa mbaya jamani.

Anonymous said...

Inanitia wasiwasi kwamba hivi magufuli ni kikwetes third term? Mbona jk analazimisha mambo Na kupindisha ukweli? Kwani lie ripoti ya CAG hajaisoma? inaianika wizara ya ujenzi chini ya magufuli kwa upovu wa mabilioni ya umma, sasa huu usafi wa kulazimisha?

Anonymous said...

Hivi wewe hujui kwamba UKAWA wameshafuta neno ufisadi kutoka kwenye kamusi ya Kiswahili tangu walipoamua kula matapishi yao? Ndiyo maana CCM haikuona sababu tena ya kutowapitisha "Mzee wa visenti" na "Mama wa million kumi ya mboga" kugombea tena ubunge kwenye majimbo yao, baada ya kushinda kwenye kura za maoni.

Anonymous said...

Hata amtambulishe kwa mungu hatupendi CCM Kama Hitler
Wazee wa Dar au kibaraka wa CCM mewagiza toka msoga hao
Mzee hasa Dar aipende CCM
No shida zote wanazozipata wengine Mafao Yao tangu Africa ya Mashariki
Hawajalipwa

Anonymous said...

Hatua Nzuri wanafanya CCM, ila nadhani kinachowashinda kuelewa ni kwamba, election ya 2015 itaamuliwa na Demograph tofauti kabisa na ambayo wao wameizoea kupata ushindi. Majority ya wapiga kura mwaka huu watakuwa ni .com generation. These are guys that they just read about Nyerere and not know who he was, they decide based on what they want and what the trend in the world goes. Ni demograph ambayo majority ni jobless, they went to school and still stays with their parents because system can not position them on formal employments.
So, talking to Dar elders as a custom is fine, but is not a winning strategy this year.
CCM if it got balls, it should face youths, and organize such youth events and try to convince them that you are with them, it is too late though.
Kwa kutumia wazee na wanawake tu CCM haiwezi kushinda uchaguzi mwaka huu, na mbaya zaidi hawataki kukubali hii fact. Ulimwenguni kote ambapo mageuzi makubwa ya kisiasa yametokea ni hii .COM generation ndio ilokuwa a changing tool. CCM ignores them or fail to persuade young Tanzanians and it will go down the same way as the other old parties around the globe goes.

Anonymous said...

Lakini jakaya, Lowassa na Lipumba si mlikuwa intenk
Moja Chou kikuu
Kulikoni
Au ndo mtaandao huu
Lakini 1995 mlikuwa nyote dhidi ya Mkapa