ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 17, 2016

MISA YA KISWAHILI - NEW YORK

Wakristu wapendwa,

Tumsifu Yesu Kristu.

Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi, wanapenda kuwatangazia ya kwamba Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la New York, limetukubalia kuanzisha Misa ya Kiswahili. 

Misa yetu ya kwanza itafanyika Jumapili, tarehe 17 mwezi wa 4, mwaka 2016, Saa 8:00mchana (Sunday 17 April, 2016, at 2 pm). Tungeomba wakristu wote watanzania na Afrika ya Mashariki wajiunge nasi katika Misa hii. Tunaomba vile vile kwa wale wanaopenda kujiunga na kwaya, basi wafike wapema kidogo, ili tufanye mazoezi kidogo, kwenye mida ya saa 7:00 mchana. 

Tunawakaribisha watu wote wanaopenda kuhudhuria ibada ya Kiswahili. 

Anwani yetu ni: Kanisa la Mt. Cecilia, 120 East 106 Street, New York, NY 10029. Between Lexington and Park Avenue. 

Chukua Train # 6. Mpaka kituo cha 110 St. Halafu tembea ukirudi mpaka 106 St.

Ni matumaini yetu kwamba mtafika kwa wingi. Karibuni tumtukuze Muumba Wetu kwa lugha yetu ya Kiswahili. 

Mbarikiwe. 

Kutoka kwa Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi....

Kwa habari zaidi unaweza wasiliana na


Mama Kintu +1-646-269-5625, au 

Ms. Doris Rweyemamu +1-646-379-9135

1 comment:

Unknown said...

Hongereni sana. Ni hatua nzuri katika kueneza kiwahili Duniani.