Mkuu wa wilaya ya nzega mkoani tabora godfrey ngupulla amewapiga marufuku wananchi wanaofanya shughuli za kuchoma mkaa na kukata mbao katika hifadhi za misitu ya serkali baada ya kubaini shughuli hizo zinafanywa katika hifadhi za serkali.
Hayo ameyasema hapo jana baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea hifadhi hizo sita za misitu zinazomilikuiwa na serkali wilyani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake mkuu huyo wa wilaya ya nzega amesema kuwa uamuzi wa kuzuia wananchi kutojishughulisha na uchomaji mkaa pamoja na ukataji mbao unatokana na kukidhiri kwa wingi ndani ya wilaya hiyo ambayo inasababisha wananchi wengi kuvamia hifadhi za serkali.
Amesema kwa sasa amepiga marufuku kutoyaona magunia ya mikaa mitaani yakitembezwa kwa ajiri ya kuuzwa pamoja na mbao,ambazo amezielezea kua ni chanzo kinachotokana na misitu ya serkali ambayo inavamiwa kila kukicha.
Ngupulla amesema mpaka sasa juhudi za kudhibiti zinaendelea kwa watu watakaobainika kujihusisha na shughuli hiyo ,huku akieleza kuwa kwa watakaobainika hatua kali zitachukuliwa ikiwemo ya kunyanganywa usafiri anaotumia kusafirisha pamoja na mzigo alionao wa mkaa au mbao.
Aidha ameendelea kusema kuwa changamoto bado zipo za kuwadhibiti watu wanaojihusisha kwa kuutumia muda wa usiku kama sehemu ya kusafirisha na kuongeza kuwa hilo wameliona na serkali wilayani humo imekua ikikabiliana nalo.
Kwa upande mwingine mkuu huyo wa wilaya,akawataka wananchi kujenga tabia ya kupanda miti mara kwa mara ili kuondokana na tatizo la wilaya hiyo kuitwa jangwa kwa kipindi kijacho.
Amesema mpaka sasa serkali imekuwa ikiwaelimisha wananchi kupanda miti kila kaya angalau miti mitano hasa ikiwemo ya matunda ili kuweza kuisaidia wilaya hiyo kuwa na miti mingi.
Amesema kwa mwaka jana walielimisha wananchi kupanda miti hivyo na kufikia idadi ya miti 2000 lakini iliyokuwa vizuri mpaka sasa ni miti 1500 na kuomba wananchi kuongeza juhudi katika kuipanda.
Naye saimoni mseti mkazi wa hapa wilayani nzega licha ya kusifu jitihada hizo za kutakiwa kupanda miti na udhibiti wa uchomaji mkaa na ukataji mbao katika hifadhi za serkali ameiomba serkali wilayni nzega kuwatatulia changamoto zinazokikabili kitengo cha misitu wilayani hapa kwa kushindwa kuwapatia wananchi mbegu mbora za matunda ambayo serkali inaomba wananchi kupanda kupanda.
No comments:
Post a Comment