ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 9, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WAKAZI WA CHATO MJINI, PIA ATEMBELEA SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA CHATO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika benchi la kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa akisafishiwa viatu  vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kukaa na  kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha Nyuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha Maalum.

No comments: