Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika mkutano aliotisha kwa lengo la kuwajulisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Simiyu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtakakatika Mkutano aliotisha kwa lengo la kuwajulisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Simiyu.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya
siku mbili Mkoani Simiyu, kuanzia tarehe
11/01/2017 hadi tarehe 12/01/2017.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari ofisini kwake leo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka amesema,
Tarehe 11/01/2017 Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa
wa Simiyu katika Mtaa wa Nyaumata Halmashauri ya Mji wa Bariadi na kufungua
barabara ya Lamadi-Bariadi.
Mtaka amesema
baada ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Mkoa na kufungua barabara ya
Lamadi–Bariadi Mhe. Rais atazungumza na
wananchi wa Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda, mahali
lilipo jiwe la ufunguzi wa barabara hiyo.
Aidha, Mtaka
ameongeza kuwa Siku ya tarehe 12/01/2017 Mhe.Rais atatembelea kiwanda cha
kutengeneza Chaki kilichopo Wilayani Maswa na baadaye ataweka jiwe la msingi
katika barabara ya Mwigumbi-Maswa ambapo pia atazungumza na wananchi wa Wilaya
ya Maswa.
“Kwa niaba ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu,napenda
kuwaalika wananchi wote wa mkoa wetu kujitokeza kwa wingi kumlaki na
kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe
Magufuli katika maeneo yote atakayopita”
amesema Mtaka.
1 comment:
safi sana
Post a Comment