Advertisements

Sunday, April 16, 2017

MISA - JUMAPILI YA PASAKA- 16 APRIL 2017

Image result for EASTER SUNDAY
Wakristu wapendwa,
Tumsifu Yesu Kristu.
Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi, wanapenda kuwatangazia ya kuwa,
Misa yetu ya kiswahili itafanyika Jumapili ya Pasaka, tarehe 16 Mwezi Aprili, 2017, Saa 8:00 mchana (Easter Sunday 16 April 2017 at 2 pm).

Tunawakaribisha watu wote wanaopenda kuhudhuria ibada ya Kiswahili, Jumapili ya Pasaka.

Anwani yetu ni: Kanisa la Mt. Cecilia, 120 East 106 Street, New York, NY 10029. Between Lexington and Park Avenue.

Chukua Train # 6. Mpaka kituo cha 110 St. Halafu tembea ukirudi mpaka 106 St.

Ni matumaini yetu kwamba mtafika kwa wingi. Karibuni sana tumshangilie Bwana, kwa lugha yetu ya Kiswahili. 

Mbarikiwe.
Kutoka kwa Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi

Karibuni...sana..tusherehekee Pasaka ya Bwana...

No comments: