Advertisements

Thursday, April 6, 2017

ROMA MKATOLIKI NA WENZAKE WAKAMATWA

Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usimsahau mchizi' amekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.
Katika taarifa iliyotolewa na msanii Prof. Jay ambay pia ni mbunge wa Mikumi inasema msanii huyo alikamatwa jana akiwa studio.
Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records.
"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi" aliandika Prof. Jay
EATV tulipojaribu kumtafuta Roma Mkatoliki simu zake zilikuwa zikiita tu bila kupokelewa.
Mpaka sasa bado hajafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi. Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

No comments: