Advertisements

Sunday, April 9, 2017

Samia Suluhu kuzindua kikosi kazi kuzuia uharibifu wa mazingira



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kwenda Iringa kesho kutwa kushiriki kikao na kuzindua kikosi kazi kuzuia uharibifu wa mazingira katika Bonde la Mto wa Ruaha Mkuu mkoani Iringa

Mbali na makamu huyo wa rais, pia wizara tano ambazo ni wizara ya Ardhi, wizara ya Maji, Kilimo na Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utali na Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) zitashiriki kikao hicho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amewaambia wanahabari leo (Jumapili) kuwa kikosi hicho kina kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mto huo.

"Hali ya uharibifu wa mazingira katika mto Ruaha Mkuu ni mbaya.Ndiyo maana Serikali imebidi ichukue hatua madhubuti ya kukabiliana na hali hii,"amesema Makamba.

No comments: