Advertisements

Sunday, June 4, 2017

WAISLAM WA NEW YORK WAJUMUHIKA NA BALOZI MERO KWENYE IFTAR

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York, Balozi Modest Mero akipata Iftar pamoja na Seif Akida, Iftar iliyoandaliwa na waislam wa New York, New Jersey na Connecticut iliyofanyika kwenye viunga vya Mt Vernon Ny na kuudhuliwa na watu mbali mbali walioko kwenye community ya Watanzania.

Mh, Balozi aliwatakia mfungo mwema waislam wote, na pia alisisitiza mshikamo na upendo bila kubaguana,  kwani Community imara  ushirikiano ni kitu muhimu sana. Hapa akiongea mbele ya Watanzania kwenye Iftar hiyo. Kwa picha zaidi nenda soma zaidi

Hapa Mheshimiwa Balozi Mero akikaribishwa na makamu mwenyeketi wa New York Tanzania Community, Gaston Mkapa.
Alhaji  Kibodja, Mkuu wa wilaya ya Springfield. MA akisalimiana na Mh. Balozi.
Masheikh wakipata futari kwenye Iftar hiyo iliyoandaliwa na waislam wa New York.Bwana Seif Akida aliefanikisha iftar hii akiongea machache mbele ya Watanzania, 


1 comment:

Anonymous said...

picha nzuri sana mmependeza sana waislamu wa new York.Allah akubarikini sana na swaumu zenu ziwe maqbool.amin.