Tuesday, September 5, 2017

UKODAK MOMENT WA OLD SCHOOL REUNION REGGAE NIGHT JUMAPLI

OLD SCHOOL REUNION COLIMBUS, OHIO

Tunapenda kukushukuru mno kwa kutenga muda na hatimae kufika kwenye Bash kongwe kupita zote OLD SCHOOL REUNION kuja kwako kumewezesha bash hii kuwa na mafanikio.

Missy T na Miss Kigoma akiwemo Miss asiyekua na Mkoa Itika, wadau kutoka Sweden na Canada kuja kwenu Columbus wakiwemo wadau wote wa Old School na wadau mbalimbali kutoka majimbo mbalimbali hapa Marekani, wachezaji wa Simba na Yanga na wachezaji wa mpira wa kikapu, wasanii bila kuwasahau wenyeji Columbus mji kipenzi kwa Watanzania.

Wote kwa ujumla wenu mmewezesha Bash hili kuwa la kihistoria. Shukurani za pekee kwa mama mitindo Asya Idarous khamsini najua hukuweza kufika lakini nia ilikuwepo.

Waandaaji hatujui tuanzie wapi kuwashukuru, kusema asante hakulingani na muda wenu na gharama nyingi mlizotumia na Columbus ikawa chaguo lenu, na OLD SCHOOL REUNION kubaki mioyoni mwenu, tunashukuru mno Mwenyezi Mungu awatangulie kwenye safari yenu, awawezeshe kufika salama na kunako majaliwa tutaonana tena. COLUMBUS OHIO  KIMATAIFA ZAIDI

SHUKRAN

DJ Luke Joe
na timu nzima ya maandalinzi
Ukodak moment kwenye zulia jekundu siku ya Jumapili Sept 3, 2017 kwenye old school reunion Columbus, Ohio.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

 


No comments: