Advertisements

Monday, February 19, 2018

MKUTANO WA UZINDUZI WA KAMPENI YA URAIS DMV

Mwanasheria wa uhamiaji Eshigo Okasili akielezea jinsi ya sheria za uhamiaji zilivyo sasa na hii ni moja ya sera za mgombea wa Urais Dj Luke ya kufanya ushirikiano wa karibu na wanasheria mbalimbali na viongozi wenzake wa Jumuiya watakapopata ridhaa ya wanaDMV katika uchaguzi utakaofanyika March 24, 2018. Moja ya sera hizo ni Jumuiya kuingia ubia na wanasheria katika kupata ushauri na mwongozo wa kisheria na maswala mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia wanaJumuiya.
Mwakilishi wa Montgomery County Heriete Shangarai akielezea faida za ushiriki kwenye mikutano yao ikiwemo kuunda ushirikiano wa miji dada kati ya county hiyo na miji ya Tanzania ambayo itawezesha kupatikana kwa huduma mbalimbali za kijamii kama vile katika sekta ya elimu na Afya
Mgombea wa Urais Dj Luke akijinadi kwa wanaDMV waliofika kwenye mkutano wake wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika siku ya Jumapili Feb 18, 2018 Silver Spring, Maryland. Mkutano huo uliohudhuriwa na wanaDMV wakiwemo wagombea wengine katika nafasi mbalimbali ambao mgombea huyo wa Urais aliwapa nafasi ya kuomba kura kwa wanDMV.

Mgombea nafasi ya makamu wa Urais Joyce Rwehumbiza Cottrel akijidadi kwa wanDMV.
Mgombea nafasi ya Ukatibu Cleopatra Kulasi akijinadi kwa wanaDMV.
Mgombea Saria Elvis akijinadi nafasi ya makamu ukatibu.
 
Mgombea nafasi ya utunza fedha Lysa Bantu akijinadi kwa wanDMV.

Mgombea Mikidadi Ali nafasi ya utanza fedha msaidizi akijinadi kwa wanDMV.
Mjumbe wa bodi  Zena Janu akijinadi kwa wanDMV

Mjumbe wa bodi  Mashaka Bilal akijinadi kwa wanDMV

Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments: