Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi kutokana kusumbuliwa na maradhi ambayo hayajawekwa wazi.
Habari za uhakika zilizoifikia MCL Digital leo Machi 5, 2018, zinasema jana alipofikishwa katika hospitali hiyo saa mbili usiku na madaktari walimwekea mashine ya kumsaidia kupumua.
Taarifa za kulazwa kwa mwenyekiti huyo ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) na Mbunge wa Hai zilianza kuzagaa leo baada ya watu kumuona hospitalini hapo.
Katibu wa Chadema mkoa Kilimanjaro, Basil Lema alipoulizwa juu ya kulazwa kwa kiongozi huyo alionekana kusita kuzungumza na kuhoji ni nani aliyetoa taarifa hizo.
Hata hivyo amesema, "Ni kweli jana aliugua ghafla na kupelekwa KCMC na madaktari walilazimika kumwekea Oksijeni ili ku stabilize (kudhibiti) afya yake lakini baadaye waliondoa hiyo Oksijeni baada ya afya yake kuimarika.”
Habari zaidi zilizopatikana zilieleza kuwa asubuhi hii madaktari bingwa wa hospitali hiyo walikuwa wakimchukua vipimo ili kubaini maradhi yanayomsumbua
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment