ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 11, 2018

BREAKING NEWS: Zesco yathibitisha kumchukua Lwandamina

Lusaka, Zambia. Uongozi wa timu ya Zambia ya Zesco United umethibitisha kupitia mtandao wake leo Jumanne kumchukua George ‘Chicken’ Lwandamina.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Katibu Mkuu wa Zesco, Richard Mulenda na kuchapishwa katika ukurasa wa Facebook wa klabu hiyo ilisema ZESCO United Football Club (FC) inayofuraha kumtangaza George Lwandamina kuwa Kocha Mkuu mpya wa klabu hii. Lwandamina anachukua nafasi ya kocha Tenant Chembo (TC) aliyetangaza kujiuzulu nafasi hiyo Jumapili Aprili 8,2018.

“Hatuna wasiwasi kuhusu uwezo, tunaamini ataendeleza rekodi yetu ya ushindi na kuendelea kutawala soka la Afrika pamoja na utamaduni wa kushinda mataji likiwa ni lengo letu kuu ZESCO United, kuanzia wachezaji hadi mashabiki.”
“ Kwa niaba ya uongozi wa klabu hiyo tunampongeza George Lwandamina kwa kuchaguliwa nafasi hiyo, pia tunawashukuru kila mmoja katika klabu yetu.” Ilimaliza kusema taarifa hiyo.

Lwandamina alitua Yanga na kuwa mrithi wa Pluijm, muda mfupi baada ya kuiongoza Zesco United kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo walitolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Mapema leo mchana mtandao wa http://zambianfootball.co.zm/ ulitoa taarifa za kuwa kocha huyo wa zamani wa Chipolopolo Boys, tayari amesaini mkataba wa awali kwa ajili ya kuchukua jukumu hilo la kuionoa timu hiyo.

Lwandamina mkataba wake na Yanga utamalizika mwisho wa mwezi Mei. Tayari kocha wa sasa wa Zesco United, Tenant Chembo amejiuzuru, lakini Katibu mkuu mpya wa klabu hiyo Richard Mulenga amesema taarifa za kujiuzuru kocha huyo ni pigo kwao.

“Jambo hili limetokea mapema sana kuhusu kujiuzulu kwa TC (Tenant Chembo).

“Tulitegemea tungekuwa naye TC hapa hadi mwisho wa Mei kabla ya Lwandamina kuchukua jukumu hilo.”

Baada ya Chembo kuondoka msaidizi wake Emmanuel Siwale anategemewa kuiongoza Zesco kesho Jumatano dhidi ya Lusaka Dynamos kwenye Uwanja wa Sunset.

MWANASPOTI

No comments: