ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 17, 2018

PICHA ZIARA YA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA MADINI KATIKA TAASISI YA GST

Mtalaam wa upimaji miamba kwa njia ya umeme Bw.Octivian Minja wa Taasisi ya jiolojia na utafiti madini (GST) mwenye shati jekundu akimuelezea Waziri wa Madini Mh.Angella Kairuki juu ya upimaji wa miamba kwa njia ya umeme kwa lengo la kujua aina ya usumaku uliopo katika miamba, waziri Kairuki tarehe 16 Mei 2018, alifanya ziara ya kutembelea GST ili kuangalia kazi mbalimbali zifanywazo na taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisis ya Jiolojia na Utafiti Madini (GST) Prof. Abdukarim Mruma alikimuelezea waziri wa Madini Angella Kairuki juu madini ya Ulanga , alipotembea katika jumba la makumbusho ya miamba na madini iliyopo GST.
Waziri wa Madini Bi.Angella Jasmine Kairuki pamoja na Manaibu waziri wa wizara hiyo Mh Dotto Biteko na Stanslaus Nyongo , na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ,wakielekea katika ofisi nyingine kwa ajili ya kutembelea baada ya kupata maelezo juu ya uchunguzi , upimaji wa miamba kutoka kwa watalaam wa Idara ya Jiofikia na Jiolojia jana tarehe 16 Mei 2018 , viongozi hao walifanya ziara ya kikazi katika Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa Madini kwa lengo la kuona kazi mbalimbali zifanywazo na taasisi hiyo.

No comments: