ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 17, 2018

Waziri Mkuu: Ajira za wageni zinazotolewa nchini ni za kitaalamu ambazo Watanzania hawana uwezo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa ajira zinazotolewa kwa wageni ni zile Kitaalum tu ambazo Watanzania hawana uwezo nazo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Mei 17, wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu ambapo pamoja na hayo ameelza kuwa wataendelea kusimamia na kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata fursa namba moja ya kuajiriwa.

“Serikali imeratibu vizuri sana suala la ajira nchini, na imetoa kipaumbele kwa Watanzania kupata ajira kwenye sekta zote nchini, wageni wanazo fursa lakini kwa masharti, ajira za wageni zote nchini ni nafasi za kitaalamu tu ambazo Watanzania hawana uwezo nazo,” amesema Waziri Mkuu.

Aidha ameongeza kuwa serikali itaendela tutaendelea suala la ajira na kuhakikisha kwamba Wtanzania wanakuwa namba moja katika kuajiriwa katika sekta zote ndani ya nchi.

No comments: