Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Slaam wakati wa majadiliano kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22); utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi. Kulia ni Mwakilishi wa UN Women nchini Bi. Susan Steffen.
Mwakilishi wa UN Women nchini Bi Susan Steffen akielezea Mipango ya Umoja wa Mataifa katika kuwezesha masuala ya Kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi wakati wa kikao kati ya Serikali na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Slaam kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) ; utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi. Kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Atupele Mwambene akielezea kuhusu utekelezaji wa Mipango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) (NPA) katika kikao kati ya Serikali na wadau kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) ; utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi.Dorah Neema akielezea kuhusu masuala ya Kamisheni ya hali ya Wanawake (CWS) katika kikao kati ya Serikali na wadau kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) , utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Vicky Makyao akizungumzia kuhusu utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi (CEDAW) katika kikao kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Maendeleo wakisikiliza kuhusu utekelezaji wa Sera, Mipango na Mikakati mbalimbali ya Serikali katika masuala ya kijinsia katika kikao kati ya Serikali na wadau kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) ; utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Serikali imekutana na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Salaam kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na Mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22); utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
Akizungumza katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga amesema Serikali imeamua kukutana na wadau ili kujadiliana na kupata maoni kuhusu utekelezaji wa Sera Mipango na mikakati ya Serikali katika masuala ya kijinsia ili kuweza kutekeleza kwa mafanikio masuala hayo.
Ameongeza kuwa Serikali inashirikiana na wadau wa Maendeleo kwa karibu ili kuwa na Mipango na mikakati ya pamoja ya kutekeleza masuala mbalimbali ya kijinsia ikiwemo kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
"Ni jambo la busara kuwashirikisha wadau wa Maendeleo katika masuala ya kimaendeleo ili kupeleke mbele kurudumu la maendeleo" alisisitiza Bi. Sihaba.
Akizungumzia utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) (NPA) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Atupele Mwambene amesema kuwa Serikali imetekeleza Mipango huo kwa mafanikio tangu kuzinduliwa kwake na masuala mbalimbali yametekelezwa katika Mipango huo ikiwemo kuwawezesha maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto iliyosaidia kupunguza vitendo hivyo hasa katika maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa UN Women nchini Bi. Susan Steffen akizungumza kwa niaba ya wadau wa Maendeleo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwashirikisha katika masuala mbalimbali ya Maendeleo na kuahidi kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali kwa manufaa ya taifa la Tanzania.
No comments:
Post a Comment