Advertisements

Monday, July 23, 2018

TANZANIA TUTALALA USINGIZI MPAKA LINI

Africa Lounge inavyoonekana picha ya pili toka kushoto inapotosha watalii wakifikiria kuwa Ngorongoro na Serengeti zipo Kenya.
Ukiwa uwanja wa ndege wa SeaTac sehemu ya kuondokea abiria utakutana na Bar moja inayojulikana kama African Lounge inayoendeshwa na  Mac na Jacks Brewing Co kutoka Redmond, WA.

Katika moja ya kuta za bar hiyo utakuta picha iliyochorwa kwa juu ikionhesha Kenya na chini ikionyesha Ngorongoro na Serengeti cha ajiaabu picha hiyo haitaji kabisa Tanzania kwa maana ya kwamba wanadanganya watalii kwamba Ngorongoro na Serengeti zipo Kenya. Angalia sehemu zilizozungushiwa kwa alama nyeusi utaelewa ninachozungumzia.

Hawa jirani zetu wameishatufanyia huu mchezo miaka mingi sana inabidi sasa tuamke tufuatilie ulimwengune kote turekebishe makosa yetu.

Anuani yao ni 17801 international blvd seattle wa 98158

Naomba Serikali iamke sasa tumechoka wenzetu kuvunia mgogoni kwetu.

No comments: