ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 5, 2018

CHIZA AAPISHWA KUWA MBUNGE WA JIMBO LA BUYUNGU.

Mbunge wa Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma Mhe. Mhandisi Christopher Chiza akiapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai Septemba 4, 2018 Jijini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimpongeza mbunge wa Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza mara baada ya kula kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai leo Bungeni Jijini Dodoma.
Sehemu ya wabunge wakifuatilia mkutano wa 12 kikao cha kwanza cha Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akiwasilisha Bungeni maelezo ya Serikali kuhusu muswaada wa sheria ya kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi wa mwaka 2018( The Dodoma Capital City ( Declaration) Bill, 2018.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali Bungeni Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwezesha mikoa kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo ili kuinua uchumi wa mikoa hiyo.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akieleza mikakati ya Serikali katika kuinua sekta ya kilimo hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mbunge wa Kibakwe Mhe. George Simbachawene akisisitiza kuhusu faida za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi yetu leo Bungeni Jijini Dodoma.(PICHA NA MAELEZO)

No comments: