Na Yeremias Ngerangera…Bagamoyo.
Mfuko wa hifadhi ya mazingira wa dunia (WWF-World Wide Fund for Nature) unaendesha mafunzo kwa viongozi wa jumuiya za uhifadhi kuwajengea uwezo wa kuimarisha mawasiliano kati ya wanajumuiya na nje ya Jumuiya. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya Millenium sea breeze mjini Bagamoyo ambapo washiriki zaidi ya 48 kutoka mikoa ya lindi ,Mtwara, Pwani na Ruvuma wanashiriki mafunzo hayo ya mawasiliano thabiti kwa lengo la kujengewa uwezo wa kufanya mawasiliano na wananchi kwenye maeneo yao ya uhifadhi .
Akifungua mafunzo hayo Drt Severin Kalonga aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kujifunza mbinu, njia na namna ya kufanya mawasiliano na jamii zilizopo katika mazingira yao ili waweze kutoa ujumbe kwa jamii ukiwa sahihi kwa watu sahihi na kwa wakati sahihi na mwishowe kupatikana kwa matokeo chanya kwa wakati. Awali Drt Kalonga aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo namna WWF inavyofanya kazi katika kuhakikisha hifadhi zilizopo zinaendelea kutunzwa na kubaini njia pekee ya kuendelea kutunza hifadhi hizo ni kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi kwa kuwa na mawasiliano yaliyorafiki na viongozi wao wa jumuiya.
Aidha Kalonga aliwaambia washiriki hao kuwa upangaji wa matumizi bora ya ardhi yanaumuhimu mkubwa katika jamii lakini akabainisha kuwa mbinu ,njia na namna ya kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa viongozi wa jumuiya akazitiia mashaka. Profesa Noah Sitati naye alisema katika uhifadhi wanakumbana na changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na shughuli za kibinadamu kama kilimo na ufugaji kufanyika ndani ya hifadhi hivyo kuathiri wanyamapori na ukataji hovyo wa misitu.
Noah aliendelea kusema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu ni lazima jamii inayozunguka hifadhi ya misitu kupewa elimu ya kutosha ya uhifadhi na faida zinazotokana na uhifadhi huo ii washiriki kikamilifu katika kulinda hifadhi za wanyamapori Pamoja na hayo alisema jamii inayozunguka hifadhi kupewa kipaumbele ili wawe mstari wa mbele katika kupambana na kutokomeza ujangili katika ngazi ya jamii.
Makamu Mwenyekiti wa WMA (wildlife management Areas) ya Jumuiya ya Mbarangandu yenye jumla ya vijiji 7katika wilaya ya Namtumbo Kassim Adam Mhagama alisema kupitia mafunzo anayoyapata atajua jinsi gani inavyotakiwa kufanya mawasiliano na watu wanaofanya nao kazi katika maeneo yake ya kazi. Mafunzo hayo ni ya siku tatu ambayo yameanza tarehe 10 Desemba na kumalizikia tarehe 12desemba mwaka huu katika ukumbi wa Millenium sea breaz Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment