Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani akiwa anajiandikisha kwenye daftari la mpiga kura katika kituo cha Msindi kilichopo katika kijiji cha Idodi kata ya Idodi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani akiwa yupo kwenye mstari kwa ajili ya kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
William Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Isimani amewataka
wakazi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga
kura kwa siku tatu ambazo zimebakia kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa
utakao fanyika tarehe 24-11-2019 na kuhakikisha wanajitokeza kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi wakati ukifika.
Akizungumza wakati
alipokuwa anajiandikisha kwenye daftari za mpiga kura katika kituo cha Msindi kilichopo
katika kijiji cha Idodi kata ya Idodi, lukuvi alisema kuwa kila mkazi wa jimbo
la Ismani wanahaki wa kujitokeza kujiandikisha na kupata haki ya kumchagua
kiongozi wanaemtaka.
“Hii ni fursa pekee ya kuhakikisha unapata
nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye atasaidia kukuletea maendeleo kwenye mtaa
au kijiji chako kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wakazi wote nawaomba
mjitokeze kwa wingi kujiandikisha” alisema lukuvi
Aidha lukuvi aliwakumbusha vijana kuhakikisha
wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha,kupiga kura na kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi
kwa kuwa nao wanahaki ya kuwa viongozi wa kuongoza mitaa ambayo wanaishi kwa
maendeleo ya jamii.
Lukuvi aliupongeza uongozi wa mkoa wa Iringa
kwa kuhamasisisha vilivyo zoezi hili la kujiandikisha kwenye daftari la mpiga
kura na kufanikiwa kuongoza kitaifa.
Nao baadhi ya wakazi wa
jimbo la Ismani waliojitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la mpiga kura
walimpongeza mbunge huyo kwa kujitokeza na kupanga kwenye mstari kwa ajili ya
kujiandikisha kwenye daftari hilo la mpiga kura.
No comments:
Post a Comment