TETEMEKO la ardhi limetokea majira ya saa 6:07 usiku wa kuamkia leo na kutikisa maeneo ya Kanda ya Ziwa hususani Masumbwe na Nyang’hwale, mkoani Geita na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa taasisi ya utafiti wa kijiolojia nchini Marekani (USGS) imesema tetemeko hilo lilikuwa lenye ukubwa wa 4.5 kwenye kipimo cha Richter.
Tetemeko hilo limezua taharuki kwa wakazi wa Geita na mikoa ya jirani, lakini mpaka sasa hakuna taarifa za madhara wala hasara zilizosababishwa na tetemeko hilo.
Mjolojia Mwandamizi kutoka taasisi ya Jiolojia Bwana Gabriel Mbogoni amesema Tetemeko hilo lina ukubwa wa 4.6 katika Vipimo vya Richta.
Bwana Mbogoni amesema Tanzania imepitiwa na mkondo wa bonde la ufa la Afrika Mashariki ikiwa na mikondo miwili mkondo wa Mashariki na mkondo wa Magharibi hivyo matukio ya mateteko ya ardhi kwenye mkondo wa bonde la ufa ni lazima yotokee na kuwataka watanzania muda wote wawe kwenye hali ya tahadhari.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita Mponjoli Lotson amethibitisha kutokea kwa tetemeko katika mkoa wake ambaye amesema Tetemeko hilo limepiga hadi Chato lakini hata hivyo haijasaabisha Madhara.
Mkoani Shinyanga hasa katika Wilaya ya Kahama ambayo inapakana na mkoa wa Geita kupitia kwa Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Anna Mringi Macha amethibitisha kutokea kwatuki hilo huku akieleza kuwa pia halijaleta madhara.

GPL
No comments:
Post a Comment