ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 25, 2020

TFF wapewa njia mbadala kumaliza ligi

By THOMAS NG'ITU

BAADA ya Shirikisho la Soka nchini Uholanzi kufuta matokeo yote ya Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Eredivisie kwa msimu huu 2019/20 na kutangaza rasmi hakutakua na bingwa wala timu iliyoshuka daraja kutokana na janga la virusi vya corona.

Wachezaji wa Ligi Kuu Bara nao wameunga mkono uamuzi huo kulingana na hali halisi ilivyo hivi sasa duniani kutokana na ugonjwa wa Covid-19 na kuipa mbinu Shirikisho la Soka nchini (TFF) namna ya kumalizia Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji wa Namungo, Blaise Birigimana amesema hali sio nzuri lakini muda mwingine inabidi iwe hivyo.

Birigimana amesema kwa upande wa Ligi ya nchini hakuna shaka Simba ndio bingwa baada ya kuwa mbele kwa pointi nyingi hivyo apewe tu ubingwa wake.

"Simba tuachane nayo maana kuna tofauti kubwa ya pointi, wa pili mpaka nne hawa watafutiwe shindano dogo kwasababu ni timu chache, wapimwe na wacheze ili ipatikane timu ambayo itamsindikiza Simba kimataifa kwasababu sina hakika kama fainali za FA kama zitakuwepo," amesema

Akizungumzia upande wa timu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), amesema huko napo wanaoongoza Ligi wapandishwe halafu wanaoshika nafasi za pili na tatu nao watafutiwe shindano lao ambalo watapimwa na kucheza bila mashabiki.

No comments: