Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoani Iringa Dr Alfredy Mwakalebela akiwa anapita katika FULL BODY MACHINE
Afisa Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa kampuni ya Asas Cosmas Charles akiwa anapita katikaFULL BODY MACHINE Afisa Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa kampuni ya Asas Cosmas Charles akimkabidhi ndoo maalum kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoani Iringa Dr Alfredy Mwakalebela
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
KAMPUNI ya Asas ya mkoani Iringa imekabidhi msaada wa mashine ya
kutakasa mwili na vifaa vingine vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya
Corona katika hospitali ya rufaa ya Mkoani Iringa.
Akikabidhi msaada huo kwa mganga mkuu wa hospitali ya rufaa mkoani Iringa, kwa niamba ya mkurugenzi uzalishaji wa kampuni ya Asas ,Afisa Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa kampuni ya Asas Cosmas Charles alisema kuwa lengo LA kutoa msaada huo ni kuhakikisha wananchi wote wanaenda katika hospitali hiyo wanajikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo vimekuwa vinahatarisha maisha ya
binadamu kote duniani.
Alisema kuwa kampuni ya Asas imekuwa ikiwakumbuka mara kwa mara wananchi katika njia tofauti ndio maana baada ya kutokea kusambaa kwa virusi vya Corona Kampuni imekuwa ikijitoa kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Iringa wanajikinga vilivyo.
Kampuni imekuwa inaendelea kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya Corona katika sekta mbalimbali hapa mkoani Iringa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaendelea kuwa salama.
Aidha Charles alivitaji vitu ambavyo kampuni ya Asas imevitoa katika hospitali ya Rufaa ya Iringa ambavyo ni mashine ya kutakasa mwili mzima,ndoo maalum 80 na barakoa 1200,Kwa upande mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoani Iringa Dr Alfredy Mwakalebela aliipongeza kampuni ya Asas kwa msaada huo walioutoa kwa kuwa ni mkubwa kulingana na mahitaji ya kujinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Mwakalebela alisema mashine hiyo ya kutakasa mwili mzima yawezekana nyanda za juu kusini ndio imekuwa ya kwanza kupatikana katika hospitali za rufaa kutoka na uhitaji wake.
"Leo tumepokea mashine hii ambayo ni bora na nzuri katika kuhakikisha tunapambana vilivyo na maambukizi ya virusi vya Corona ambvyo vimekuwa vikishia uhai wa binadamu kote duniani"
alisema Mwakalebela alisema kuwa licha ya kutoa mashine hiyo lakini kampuni ya Asas imetoa pia ndoo maalum 80 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona pamoja barakoa 1200.
No comments:
Post a Comment