Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, umefikishwa nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa kwa ajili ya taratibu za kuuaga kabla ya kuelekea eneo alipozaliwa Tosamaganga nje kidogo ya mji wa Iringa kwa ibada ya mazishi.
Balozi Dkt Mahiga alifariki dunia alfajiri ya jana Ijumaa, Mei 1, 2020 baada ya kuugua ghafla akiwa mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment