ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 7, 2020

Kuwalaza wagonjwa kifudifudi husaidia kuokoa maisha yao

Na MWANDISHI WETU, Mtanzania

KUJIKUTA katikati ya mgogoro unaosababishwa na janga la corona, ni tukio ambalo mara kwa mara hufanyika katika hospitali nyingi duniani.

Makumi ya wagonjwa husalia kwenye vitanda vyao, wakiwa wamewekewa vifaa vya kuwasaidia kupumua huku wakiangaliwa kwa makini na maafisa wa afya ambao hulindwa na nguo maalum pamoja na barakoa.

Lakini kuna kitu ambacho kinavutia katika picha hizi, baadhi ya wagonjwa wanaougua covid 19 hulazwa kifudifudi.

Sababu kulazwa kifudifudi

Wataalamu wa masuala ya afya wanadai kuwa kufanya hivyo kunaongeza kiwango cha oksijeni mwilini. Ni mfumo wa jadi ambao umethibitisha kufanya kazi kukabiliana na magonjwa hatari ya mapafu.

Mbinu hiyo inayojulikana katika taaluma ya afya kama kulala juu chini, imeanza kutumiwa kwa kiwango kikubwa miongoni mwa maelfu ya wagonjwa ambao ni waathiriwa wa mlipuko corona wanaoendelea kutibiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Mbinu hii husaidia watu kuimarisha kiwango cha oksijeni kinachoingia katika mapafu.

Profesa wa tiba ya mapafu na chumba cha wagonjwa mahututi katika Chuo Kikuu cha Tiba cha John Hopkins, Panagis Galiatsatos, ameileza BBC kuwa wagonjwa wengi walioathirika na virusi vya corona hawapati oksijeni ya kutosha katika mapafu yao na hivyo huyaharibu.

“Na ijapokuwa tunawapatia oksijeni katika vituo vya afya, mara nyingi huwa haitoshi. Tunachofanya ni kuwalaza kifudifudi ili kuruhusu mapafu kupanuka tena,” anasema.

Mtafiti huyo anaongeza kwamba maeneo mazito ya mapafu huwa yako mgongoni hivyo basi mgonjwa anapolalia mgongo wake tatizo la wao kushindwa kupumua huongezeka.

Husaidia damu kusambaa

“Kufunguka kwa mapafu wakati mgonjwa anapolalishwa kifudifudi husaidia kusambaa kwa damu zaidi. Mbinu hiyo ina ufanisi na tumeithibitisha kwa wagonjwa wengi.

”Mbinu hiyo imetambulika na madaktari wengi hali ya kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) pia limeipendekeza Machi, mwaka huu, kwa wagonjwa wanaougua Covid-19 ambao wanaugua magonjwa ya tatizo la kupumua,” anasema.

Cha zaidi ni kwamba uchunguzi uliofanyiwa wagonjwa 12 waliokuwa katika hali mahututi waliotibiwa katika hospitali ya Jinyintan nchini China, ulibaini kwamba wagonjwa ambao hawalazwi kifudifudi mapafu yao hukosa kupanuk

No comments: